Pata taarifa kuu
SHERIA-HAKI

Chad: Mahakimu wasitisha mgomo wao

Baada ya miezi miwili ya kusitisha shughuli za mahakama ili kudai kuboreshwa kwa hali ya maisha na kazi zao, mahakimu wamesitisha mgomo wao. Hawajapata chochote madhubuti isipokuwa ahadi ya kurejelewa upya kwa mishahara yao kuanzia mwezi wa Januari 2023.

Mahakama moja huko Ndjamena.
Mahakama moja huko Ndjamena. AFP - PASCAL GUYOT
Matangazo ya kibiashara

Jumanne hii, Novemba 08 inaonekana kama siku ya uamuzi katika mahakama mbalimbali nchini Chad. Ofisi zilizofungwa kwa miezi miwili zimefunguliwa tena. Usafi umefanywa katika mahakamahizo, faili zilizoachwa zimechukuliwa. Kwa kweli, kazi itaanza tena kwa siku chache, Kwa sasa mambo ya kiufundi ndio yanaangaliwa zaidi.

Bruno Taoka, kiongozi wa chama kinachojiendesha cha mahakimu nchini Chad anaeleza: “Leo, katika ngazi ya ofisi za mashtaka zitapokea tu malalamiko na kisha kesi zitapangwa kusikilizwa katika siku za hivi karibun. Kwa wale ambao walikuwa wakisubiri kuachiliwa, maagizo ya mwisho ya kuachiliwa pia yatatiwa saini na mwendesha mashtaka. "

Siku ya Ijumaa, vyama viwili vya mahakimu vilikuwa na kikao kirefu cha kazi na Waziri Mkuu ambacho kiliwawezesha kupata baadhi ya matokeo.  "Pande hizo mbili zilihitimisha kikao chao kwa kusaini hati ya makubaliano ambayo ilikuwa ni suala la kukubali 50% kuhusiana na posho na agizo la kiwaziri ilitiwa saini na Waziri Mkuu kupitia upya jinsi mahakimu wanavyoshindana daraja" ameongeza Bruno Taoka.

Mgomo huo umesitishwa kwa muda wa miezi mitatu na huenda ukaanza tena mwishoni mwa mwezi wa Januari 2023, kulingana na vyama vya mahakimu, ikiwa serikali haitatimiza ahadi zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.