Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Rais Cyril Ramaphosa akutwa na Covid-19

Baada ya kupimwa na kukutwa na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 Jumapili hii, Desemba 12, Rais wa Afrika Kusini anaendelea kupatiwa matibabu.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwa kanisani mjini Cape Town Desemba 12, 2021, wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Frederik de Klerk.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwa kanisani mjini Cape Town Desemba 12, 2021, wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Frederik de Klerk. REUTERS - MIKE HUTCHINGS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili asubuhi, Rais Cyril Ramphosa, 69, alitoa hotuba mbele ya watu wapatao 200 katika kanisa moja mjini Cape Town akitoa heshima ya mwisho kwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Frederik de Klerk.

Maambukizi yake yanakuja wakati Afrika Kusini inakabiliwa na mlipuko wa nne wa janga linasababishwa na kirusi kipya cha Omicron.

Hotuba yake ya kumuaga Frederik de Klerk, mbele ya mamia ya watu Jumapili, Desemba 12, ilikatizwa na kikohozi. Jioni, ofisi ya rais wa Afrika Kusini ilibaini kwamba Cyril Ramaphosa alipimwa na kukutwa na Covid-19. Alikuwa ameanza kujisikia vibaya alipotoka kwenye sherehe.

Ofisi ya rais inawashauri watu ambao walitangamana naye kufuatilia afya zao na kupima. Katika taarifa yake, Rais Ramaphosa almesema anataka maambukizi yake yawe onyo la kuwahimiza watu kuwa makini.

Afrika Kusini ndiyo kitovu cha mlipuko wa nne wa janga linalosababishwa na kirusi kipya cha Omicron, kilichogunduliwa nchini humo mwishoni mwa mwezi Novemba. Kesi mpya 18,000 bado zimetambuliwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Zaidi ya robo ya vipimo vimethibitishwa kuambukizwaugonjwa huo.

Cyril Ramaphosa alirejea nchini hivi karibuni baada ya kufanya ziara katika ukanda wa Afrika Magharibi, iliyomalizika Desemba 8, baada ya kuzuru nchi nne. Katika tukio hili, alikuwa amefanyiwa vipimo mara kadhaa. Hakuna maambukizi yaliyopatikana. Rais Ramaphosa anakumbusha kwamba alichanjwa na kwamba raia wenzake wanapaswa kufanya hivyo. Ni 37% tu ya watu wazima waliopewa chanjo. Afrika Kusini ndiyo nchi iliyoathiriwa zaidi katika bara la Afrika ikiwa na vifo 90,000 na maambukizi milioni 3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.