Pata taarifa kuu
AFYA-USHIRIKIANO

WHO yataka kuepo na makubaliano ya kupambana na magonjwa ya milipuko

Shirika la Afya Duniani, WHO, linakutana katika kikao maalum kuunda mkataba juu ya milipuko wa Covid-19. WHO pia imepinga vikwazo vinavyoathiri kusini mwa Afrika baada ya ugunduzi wake juu ya aina mpya ya kirusi cha Omicron.

Makao makuu ya Shirika la Afya Duniani huko Geneva, Mei 19, 2020.
Makao makuu ya Shirika la Afya Duniani huko Geneva, Mei 19, 2020. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya pili katika historia yake kwa WHO kukutana katika kikao maalum, ameeleza mwanahabari wetu mjini Geneva, Jérémy Lanche. Hii inakuja katikati ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona huko Ulaya, na siku chache tu baada ya wanasayansi wa Afrika Kusini kugundua uwepo wa aina mpya ya kirusi cha Omicron.

Wakati Mataifa mengi zaidi yanajizuia katika kukabiliana na tishio hili jipya, WHO inatoa wito badala yake kuacha mipaka wazi, hasa na Afrika Kusini. Kwa upande wa shirika la Afya Duniani, hatua hizi hazina tija.

Ikiwa nchi itatangaza kuibuka kwa aina mpya ya kirusi kwenye ardhi yake, na kwamba kwa kujibu haua za kuitenga zinachukuliwa, basi ni kusubiri hatari katika siku zijazo, nchi hazitashirikiana kwa uwazi. Aidha, vikwazo hivi havijazuia tofauti ya B1.1.529 kuenea, kwa kuwa tayari imetambuliwa katika mabara kadhaa ya dunia.

Kutokana na tishio hili ambalo bado linaweza kupimwa kwa usahihi si maambukizi au ugonjwa, kwa kukosa mtazamo, WHO inasihi kuchunguzwa upya kwa mikataba ya kimataifa inayoelekea ushirikiano zaidi. Hii ndiyo maana halisi ya kikao.

Kwanza, kuna suala la upatikanaji wa chanjo: ikiwa hakuna usawa katika kugawana chanjo, na nchi zilizohifadhiwa kwa upande mmoja na nchi mbazo inasema virusi vinazunguka kwa upande mwingine, hii kwanza inaleta tatizo la kimaadili, na hii ni kuchukua hatari ya kuona aina mpya ya kirusi inaibuka. WHO imekuwa ikionya kuhusu hili kwa miezi kadhaa. Omicron inaonyesha kwamba matokeo yalikuwa sahihi, anabainisha Simon Rozé, anayesimamia maswali ya kisayansi katika RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.