Pata taarifa kuu
INDIA-JAMII

India: Modi atangaza kufutwa kwa sheria za mashamba kwa madhumuni ya uchaguzi

Waziri Mkuu wa India ametangaza hivi punde kwamba ataomba kuondolewe kwa sheria tatu zenye utata za mageuzi ya kilimo. Haya yanajiri baada ya maamndamano makubwa ya wakulima yaliyodumu kwa miezi kumi na tano na kusababisha vifo vya zaidi ya wakulima 700. Kwa hivyo serikali inarejelea sheria hii kwa mara ya kwanza, hasa kwa madhumuni ya uchaguzi.

India itafuta sheria tatu za mageuzi ya mashamba ambazo zimesababisha takriban mwaka mmoja wa maandamano makubwa ya wakulima, Waziri Mkuu Narendra Modi amesema.
India itafuta sheria tatu za mageuzi ya mashamba ambazo zimesababisha takriban mwaka mmoja wa maandamano makubwa ya wakulima, Waziri Mkuu Narendra Modi amesema. Sajjad HUSSAIN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Ustahimilivu wa wakulima umezaa matunda. Baada ya miezi kumi na tano ya kustahimili baridi kali na kisha joto kali la mjini New Delhi, mji mkuu wa India, hatimaye serikali imekubali shinikizo lao. Hii ni mara ya kwanza katika miaka saba Narendra Modi akirejelea hatua ya mageuzi makubwa. Waziri Mkuu anasema anafanya hivyo kwa sababu hangefaulu kuwashawishi "baadhi ya wakulima", lakini lengo halisi ni dhahiri: maandamano ya wakulima yanaweza kukipeleka pabaya chama chake katika uchaguzi ujao huko Uttar Pradesh, jimbo la vijijini na kubwa zaidi nchini.

Modi ametoa tangazo hilo la kushtukiza wakati wa hotuba ya televisheni iliyorushwa moja kwa moja.

"Katika miezi ya hivi karibuni, wakulima pia wamefanya vitendo vya kuharibu shughuli za kampeni za chama cha BJP," aamesema mtaalam wa masuala ya siasa Gilles Verniers, mkurugenzi wa Kituo cha Uchambuzi wa Data katika Chuo Kikuu cha Ashoka, karibu na mji wa New Delhi. Na hiyo imekuwa inakera kwa shughuli za uchaguzi za chama cha BJP, tatizo ambalo lilihitaji kuondolewa. Lakini kwa maoni yangu, kuna mambo mengine ambayo pia yanahusika: kipindi hiki kilikuwa tukio kubwa kwa vyombo vya habari vibaya kwa Modi na kwa India kwa ujumla, katika vyombo vya habari vya kimataifa. Na pia kuna ukweli kwamba sheria hizi, hata hivyo, hazingetekelezwa, tangu Mahakama ya Juu ilipozisimamisha mwezi Januari mwaka huu, ikiomba serikali kutafuta suluhu na wakulima. Lakini wakulima walishikilia msimamo wao ... Kwa hivyo badala ya kuendelea kushinikiza sheria ambazo kwa wazi hazingeweza kutekelezwa, inaweza kuwa busara zaidi kufumbia macho sasa na kuondoa tatizo hilo ”.

"Ni ushindi, lakini Modi atabaki kuwa mhalifu wa maandamano haya ya kilimo," Kamaljeet Singh, msemaji wa chama cha wakulima cha Punjab Kisan Union. Madai yetu hayajabadilika tangu siku ya kwanza, lakini alisubiri zaidi ya mwaka mmoja kubadili mageuzi haya, na zaidi ya wakulima 700 walikufa barabarani. Hivi ndivyo Modi alifanya, hakuondoa mageuzi haya, lakini alichelewesha uondoaji huu kwa mwaka mmoja. "

Modi amesema mchakato wa kikatiba wa kuondoa sheria hizo utaanza Desemba wakati bunge litaanza vikao vyake vya msimu wa baridi.

Sheria hizo zilipitishwa Septemba mwaka jana na serikali ikazitetea, ikisema zilikuwa muhimu kuimarisha sekta ya kilimo ya India na itaongeza uzalishaji kupitia uwekezaji wa kibinafsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.