Pata taarifa kuu

Covid-19: WHO yatoa idhini ya dharura kwa chanjo ya India ya Covaxin

Shirika la Afya Duniai, WHO, limetoa idhini ya dharura kwa chanjo ya Covaxin ya kupambana na Covid-19 kutoka maabara ya India ya Bharat Biotech.

Chanjo hii - yenye uwezo wa 78% - inapendekezwa kwa makundi yote ya umri kutoka miaka 18.
Chanjo hii - yenye uwezo wa 78% - inapendekezwa kwa makundi yote ya umri kutoka miaka 18. Prakash Singh AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inatoa hakikisho kwa chanjo ambayo mamlaka nchini humo zilikuwa tayari zimeruhusu kutumika kitambo kabla ya kukamilishwa kwa vipimo vya usalama na ufanisi.

Hatua hiyo inaifanya Covaxin kuwa chanjo ya nane ya kupambana na COVID-19 kupewa idhini na WHO.

Chanjo hii - yenye uwezo wa 78% - inapendekezwa kwa makundi yote ya umri kutoka miaka 18. Inahitaji dozi mbili kwa wiki nne tofauti lakini "inafaa hasa kwa nchi za kipato cha chini na cha kati kwa sababu ya urahisi wa kuihifadhi," kulingana na taarifa ya WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.