Pata taarifa kuu
INDIA-AFYA

Covid-19: India kunza kuchanja bure watu wazima

Serikali ya India imetangaza kuwa watu wazima wote wataweza kupata chanjo ya Covid-19 ya bure. Haya ni mabadiliko makubwa katika sera inayoendelea hadi sasa, inayokosolewa na upinzani na Mahakama Kuu.

Hatimaye dozi zitanunuliwa na serikali ya shirikisho, India, ili kutoa chanjo ya bure kwa watu wazima.
Hatimaye dozi zitanunuliwa na serikali ya shirikisho, India, ili kutoa chanjo ya bure kwa watu wazima. AP - Mahesh Kumar A
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Mei 1, serikali ya shirikisho ilifungua chanjo kwa watu wazima walio chini ya umri wa miaka 45, lakini dozi hizi mpya zilitarajiwa kununuliwa moja kwa moja na serikali za majimbo na hospitali za kibinafsi. Hatua ambayo ilizua hofu kwa sababu mikoa thelathini ilishindana katika ununuzi huu na hospitali za kibinafsi, ambazo ziliweza kuuza kwa bei ghali chanjo hiyo,  na kuweza kutoa huduma iliyo bora zaidi.

Chanjo hiyo ilipowasili, serikali za majimbo kwa ujumla zilitoa chanjo za bure, lakini zilikosa dozi ya kutosha katika wiki za hivi karibuni, wakati hospitali za kibinafsi zinaendelea kutoa chanjo, lakini kwa karibu euro 10 kwa kila dozi. Upinzani ulilalamikia sera hiyo na Mahakama Kuuiliitaja sera hiyo kuwa isiyo na mantiki na ya kibaguzi.

Kwa hiyo New Delhi imejirudi na kuamua kwamba serikali kuu itanunuwa chanjo hiyo na kuitoa bure kwa watu wazima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.