Pata taarifa kuu
INDIA-AFYA

Covid-19: India yavuka kizingikiti cha vifo 300,000

India imetangaza leo Jumatatu kuwa imevuka kizingiti cha vifo 300,000 kutokana na Corona, na kuwa nchi ya tatu duniani kufikia takwimu hii, baada ya Marekani na Brazil.

India imevuka kizingiti cha vifo 300,000 kutokana na Corona Jumatatu, Machi 24. Pich hii inaonyesha mazishi ya watu waliofariki kutokan ana Corona huko Hyderabad, Mei 23.
India imevuka kizingiti cha vifo 300,000 kutokana na Corona Jumatatu, Machi 24. Pich hii inaonyesha mazishi ya watu waliofariki kutokan ana Corona huko Hyderabad, Mei 23. AP - Mahesh Kumar A
Matangazo ya kibiashara

Katika wiki za hivi karibuni, India ilirekodi mara kwa mara idadi ya kila siku ya visa vya maambukizi na vifo. Idadi ya visa vya maambukizi imezidi milioni 26.7, idadi inayoshangaza, hata ikilinganishwa na idadi ya watu wote: wakazi bilioni 1.3.

Na kwa muda wa saa 24 zilizopita, nchi hiyo ilirekodi vifo vipya 4,454 kutokana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, ikiwa ni ripoti ya pili ya kila siku ya idadi ya juu zaidi tangu rekodi ya vifo 4,529 kufikia siku ya Jumatano, limebaini shirika la habari la AFP. Lakini kulingana na wataalamu, takwimu hizi bila shaka siza kweli na wanona kua idadi iko juu zaidi kwani maambukizi zaidi pia yanaripotiwa vijijini.

Maiti za watu wanaoshukiwa kuwa waathiriwa wa Corona zilipatikana zikielea kwenye maji ya Ganges au kuzikwa kwenye makaburi ya kina kirefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.