Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Watu waendelea kuuawa mashariki mwa DRC, wanaharakati walalama

Watu 16 wameuawa kwa kuchomwa visu na waasi wanaoaminiwa kuwa wa ADF katika barabara ya Idohu katika mkoa wa Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kutekwa.

Ramani ya Ituri na vijiji vya Boga na Tchabi ambapo mashambulizi mabaya yamefanyika hivi karibuni.
Ramani ya Ituri na vijiji vya Boga na Tchabi ambapo mashambulizi mabaya yamefanyika hivi karibuni. © baromètre sécuritaire du Kivu
Matangazo ya kibiashara

Jeshi na maafisa wa serikali wanasema mauji hayo yalitokea siku ya Jumatatu na miongoni mwa waliouwa ni wanawake wawili waliokuwa wametekwa wiki kadhaa zilizopita na waasi hao.

Wakati hayo yakijiri, mashirika ya kiraia, yanalalamikia ongezeko la mauaji ya raia katika mkoa huo wa Ituri. Shirika la CEPADHO linasema kwa kipindi cha siku 10 zilizopita, watu 42 wameuawa sawa na wengine 332 Wilayani Irumu na wengine 165 huko Beni.

Shirika la LUCHA sasa linataka kuondolewa kwa Gavana wa kijeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini likibaini kwamba hawajibiki katika majukumu yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.