Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI

DRC: Maafisa kadhaa wa jeshi la FARDC wakamatwa kwa madai ya ubadhirifu

Wanajeshi sita, ikiwa ni pamoja na maafisa waandamizi wa jeshi la DRC walioko Beni, mashariki mwa nchi hiyo wako chini ya sheria ya mahakama ya kijeshi tangu Jumanne (Julai 27).

Wanajeshi wa DRC katika kijiji cha Manzalaho karibu na Béni Februari 2020 (Picha ya zamani).
Wanajeshi wa DRC katika kijiji cha Manzalaho karibu na Béni Februari 2020 (Picha ya zamani). AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na msemaji wa Ukaguzi Mkuu wa jeshi la FARDC, wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa pesa zilizokusudiwa wanajeshi waliopelekwa mashariki mwa DRC kama sehemu ya mapambano dhidi ya makundi yenye silaha.

Hii ni sehemu ya operesheni ya ukaguzi uliozinduliwa zaidi ya wiki moja iliyopita, na ambayo inahusu mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini, iliyowekwa chini ya amri ya kijeshi. Kabla yao, maafisa wengine 11 walikamatwa huko Bunia.

Kanali Polydor Lumbu Mutindu anayehusika na maswala ya utawala katika Sekta ya utendaji ya Sukola 1 Grand Nord na maafisa wanne ni miongoni mwa maafisa hao wa jeshi waliowekwa chini ya sheria ya mahakama ya kijeshi.

Majina ya majenerali

Kulingana na msemaji wa Ukaguzi Mkuu wa Jeshi, wote wanahusika katika ubadhirifu uliothibitishwa. Maafisa hawa watakabidhiwa kwa mkaguzi mkuu huko Goma kwa. Hata hivyo operesheni hiyo bado inaendelea.

Ukaguzi Mkuu wa Jeshi umeahidi kuweka wazi kila kitu ifikapo Jumamosi, wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Majina ya baadhi ya majenerali, ambao wanakabiliwa na mashaka makubwa ya ubadhirifu, yatatangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.