Pata taarifa kuu
DRC-KILIMO-UCHUMI

Nzige wa jangwani wavamia Mashariki mwa DRC

Kwa sasa ni wilaya tu ya Aru katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo, iliyoathiriwa na nzige hao wa jangwani. Lakini wadau mbalimbali katika nchi hiyo wanasema wana wasiwasi na uvamizi huo unaoendelea katika nchi mbalimbali za Afrika.

Kundi la nzige wa jangwani linazunguka kando ya kijiji cha Lerata, kilomita 300 kutoka Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Kundi la nzige wa jangwani linazunguka kando ya kijiji cha Lerata, kilomita 300 kutoka Nairobi, mji mkuu wa Kenya. AFP/Tony Karumba
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Kenya, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, Sudani, Tanzania na Uganda, mashariki mwa DRC sasa inakabiliwa na uvamizi wa nzige wa jangwani. Kulingana na vyanzo kadhaa kutoka Ituri, nzige wa jangwani walivamia wilaya ya Aru Februari 19.

Kwa sasa, hakuna hatua thabiti ambayo imechukuliwa ili kukabiliana na uvamizi huo.

Hata hivyo tishio bado lipo, ameonya Dieudonné Lossa, kiongozi wa chama cha wahandisi wa kilimo mkoani Ituri.

"Kinachotia wasiwasi sana kwanza ni uharibifu ambao wadudu hao watasababisha kwa mazao. Raia watapoteza mazao. Mashamba yao yatateketezwa. Kuna hatari ya kupoteza kila kitu. Kuna hatari ya kutokuwa na chakula chochote katika jiji la Bunia na Ituri kwa ujumla, " amesema Guerschom Dramani Pilo, Waziri wa Kilimo katika Mkoa wa Ituri amesema.

Bila kukana tishio ambalo nzige hawa husababisha kwa kilimo, mamlaka mkoani Ituri wanahakikisha kwamba hali hiyo bado inaweza kudhibitiwa.

Waziri wa Kilimo katika Mkoa waIturi amesema kuwa timu ya wataalamu imepelekwa katika eneo la Aru ili kutathmini hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.