Pata taarifa kuu
DRC-BENI-MAUAJi-USALAMA

Kumi na tano wauawa katika shambulio la ADF Alungupa, DRC

Raia kumi na tano wameuawa na zaidi ya kumi wametekwa nyara katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na waasi wa Uganda wa ADF usiku wa Jumatatu, Februari 17 huko Alungupa katika sekta ya Rwenzori, wilayani Beni.

Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimama karibu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmoja huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018.
Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimama karibu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmoja huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa karibu saa 4 usiku wakati waasi hao walivamia kijiji hicho. Kulingana na vyanzo kutoka eneo hilo, raia kumi na tano waliuawa na wengine kumi kutekwa, wakiwemo watano kutoka familia moja. Wakazi kadhaa wa kijiji hicho pia waliporwa mali zao. Waasi walpora ng'ombe na vitu vya thamani, kwa mujibu wa vyanzo hivyo.

Naibu msemaji wa jeshi la DRC, FARDC, Brigadia Jeneral Sylvain Ekenge, amethibitisha habari hii, kwa mujibu wa Radio ya Umoja wa mataifa Okapi. Lakini, ametoa idadi ya watu saba waliouawa. Brigadia Jeneral Sylvain Ekengena amehakikisha kwamba jeshi linamsaka adui.

Kwa upande wake, shirika la kiraia katika wilaya ya Beni limeomba jeshi kupitia mkakati wake, kwenye barabara na maeneo waawi wanakojificha.

Janvier Kasahiryo, msemaji wake wa shirika hilo, anahofia kwamba hali hii, ikiwa itaendelea, itaathiri jiji la Butembo. Hata hivyo, ametolea wito viongozi kuhamasisha vijana kuendelea kuwa kudumisha msikamano na kuimarisha ulinzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.