Pata taarifa kuu
DRC-MAUAJi-USALAMA

Raia waendelea kuuawa Mashariki mwa DRC

Watu saba wameuawa katika mauaji mapya, yaliyotekelezwa na waasi wa Uganda wa ADF Nalu katika Wilaya ya Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Askari wa vikosi vya Umoja wa Mataifa huko Beni, DRC, Novemba 26, 2019.
Askari wa vikosi vya Umoja wa Mataifa huko Beni, DRC, Novemba 26, 2019. ALBERT KAMBALE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamethibitisha kutokea kwa mauaji haya katika eneo la Makeke, Kaskazini mwa Beni baada ya waasi wa ADF wanaominuwa kuwa zaidi ya 60 kuvamia eneo hilo na kuanza kuteketeza mauji hayo.

Wanaume watano na wanawake wawili ndio waliouawa na walioshuhudia wanasema, mauaji hayo yalifanyika mchana jana Jumapili, huku waasi hao wakiteketeza moto maduka matano.

Mauaji haya yametokea baada ya miili ya watu wengine 12 kupatikana karibu na mji wa Beni Ijumaa iliyopita, lakini pia watu wengine wanane kuuliwa na wengine 20 kutoweka.

Hayo yanajiri wakati wakaazi wa mji wa Mangina Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameukimbia mji huo ulioko katika eneo la Beni, baada ya mfululizo wa mashambulio yaliyosababishwa na waasi wa kundi la ADF, kwa mujibu wa duru tawala.

Kwa mujibu wa viongozi wa mashirika ya kiraia takriban watu thelathini wameuawa mwishoni mwa juma hili.

Sehemu kubwa ya wananchi wa Mangina wameukimbia mji huo kwa mujibu wa Muhindo Musubao, naibu mwenyekiti wa mashirika ya kiraia katika mji wa Mangina.

Mauji yameendelea kuripotiwa katika eneo la mashariki mwa Congo na kusababisha wananchi wa maeneo hayo kukataa tamaa kutokana na mwendelezo wa mauaji hayo huku wengine wakilamika kutoroka makwao.

Tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita, mamia ya raia wamepoteza maisha Wiyani Beni, Mashariki mwa nchi hiyi, licha ya jeshi la serikali na lile la Umoja wa Mataifa kusema kuwa yanashirikiana kwa kupambana dhidi ya waasi hao.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa tangu Oktoba mwaka jana watu zaidi yta 300 wamepoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.