Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI-UFISADI

DRC yaweka mpango wa matumizi ya fedha kwa kuzuia pesa kupotea

Serikali ya DRC imetoa mpango wa matumizi ya fedha, mpango ambao utasaidia kurekebisha matumizi ya serikali, baada ya kupotea kwa Mamilioni ya dola mwaka 2019.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa DRC, Kinshasa (picha ya kumbukumbu).
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa DRC, Kinshasa (picha ya kumbukumbu). John Wessels/Bloomberg via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni shirika la Fedha Dunia (IMF) liliomba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuonyesha ukweli katika matumizi yake ya fedha za umaa.

Mbali na bajeti ya kihistoria ya kiwango cha juu ya dola bilioni 11, zilizotangazwa hapo miezi miwili iliyopita na rais Tshisekedi, mpango huu wa kuzuia pesa kupotea unatoa nusu ya mapato; na, hadi leo, nusu ya matumizi ya fedha.

DRC imepanga kutumia dola bilioni 5.64 na serikali inaamini inaweza kupata dola bilioni 5.4 katika mapato yake. Upungufu wa milioni 200 unatarajiwa kujazwa na feza zitakazotolewa na Benki Kuu.

Uchunguzi kuhusu matumizi ya pesa yanayo fanyika ikulu nchini DRC, ulibaini kwamba ikulu ilitumia pesa nyingi kwa kipindi cha muda mchache kiasi kwamba, tangu rais Felix Tshisekedi aingie madarakani, pesa zinazotakiwa kutumika ikulu kwa muda wa mwaka mzima, zilitumika na kuisha kabisa kwa muda wa miezi 5 pekee ambayo rais amekaa madarakani.

Kesi hii ya kupotea kwa Dola Milioni 15 ilizua hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku mashirika ya kiraia yakiomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kupata ukweli wa mambo.

Wakati huo huo wakosoaji wa Mkurugenzi wa ofisi ya rais, Vital Kamerhe, walimuhusisha kiongozi huyo kwa kesi hiyo, licha ya yeye kufutilia mbali tuhuma hizo.

Kupotea kwa fedha hizo kuliibua maswali mengi kati ya mashirika mbalimbali na wakosoaji wa serikali ya DRC.

Vital Kamerhe ambaye wakosoaji wake wanamwita "rais wa pili" alipuuzia mbali madai hayo akisema kuwa lengo la wapinzani wake ni kumchafua tu.

Vital Kamerhe ni miongoni mwa viongozi wanne ambao Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali unawahusisha katika kesi hiyo ya kupotea kwa dola Milioni 15.

Katika mahojiano na Gazeti la Jeune Afrique, Vital Kamerhe, Mkurugenzi wa ofisi ya Rais Félix Tshisekedi, alifutilia mbali kuhusika kwake katika kesi hiyo na alikanusha suala la "kupotea kwa fedha hizo", na kusema kuwa kesi hiyo "ilisitishwa" na Mkaguzi Mkuu wa kitengo cha Uhalifu wa Uchumi.

Vital Kamerhe pia alisitisha uchunguzi mwingine uliozinduliwa na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (IGF), ikiwa ni pamoja na uchunguzi kuhusu matumizi yote kwenye wizara mbalimbali tangu Felix Tshisekedi kuchukuwa madaraka, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka serikalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.