Pata taarifa kuu
LIBERIA

LIBERIA: Marekebisho katiba, hofu kuhusu rais Weah kuwania kwa muhula wa 3

Raia wa Liberia, siku ya Jumanne watapiga kura ya maoni kupunguza muda wa rais kukaa madarakani, pendekezo ambapo wapinzani wa rais George Weah, wanoana analenga kutumia mwanya wa merekebisho ya katiba kugombea tena.

Rais wa Liberia, George Weah.
Rais wa Liberia, George Weah. Photo: Ludovic Marin/Pool/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika kura hiyo, wananchi wataulizwa pia kuhusu suala la uraia pacha, suala lililozua mjadala mkubwa kwenye moja ya taifa masikini duniani.

Weah ambaye ni mchaza soka wa zamani, anataka kupunguza muda wa rais kukaa madarakani pamoja na kupunguza idadi ya wabunge kutoka miaka 6 hadi 5 na kutoka maseneta 9 hadi 7.

Weah, juma lililopita, akihutubia wafuasi wake aliwaambia “Mimi naamini kumuweka mtu madarakani kwa muda mrefu sio njia sahihi ya kwenda,”

Hata hivyo suala la kupunguza muda wa rais kukaa madarakani ni jambo linaloonekana jipya kwenye mataifa mengi ya ukanda wa Afrika Magharibi, ambapo viongozi wengi wameshabadili katiba kujiongezea muda zaidi.

Nchini Guinea kwa mfano, rais Alpha Conde, mwenye umri wa miaka 82 hivi sasa alishinda muhula watatu wa urais katika uchaguzi wenye utata mwezi Octoba, baada ya kufanikiwa kupitisha mabadiliko ya katiba kuruhusu kugombea kwa mihula zaidi ya miwili.

Hali kama hiyo imeshuhudiwa nchini Ivory Coast, ambapo rais Alassane Ouattara, alishinda kwa muhula watatu kiti cha urais katika uchaguzi wenye utata baada ya awali kuwa alipitisha marekebisho ya katiba.

Hofu ya Muhula watatu:

Wakosoaji wa rais Weah, wana hofu kuwa huenda kiongozi wao akatumia njia hiyo hiyo ya marekebisho ya katiba.

“Rais George Weah, lazima atataka kugombea kwa muhula watatu, kwa kuwa miaka sita ya awali itakuwa haimzuii tena katika marekebisho haya ya katiba ya muda wa miaka 5”, alisema seneta wa upinzani Darius Dillon.

Dillon, anasema kura ya ‘Ndio’ itakuwa ni makossa makubwa.

Akikulia katika jiji kuu la Monrovia kabla ya kung’ara katika soka na klabu ya AC Milani na PSG, Weah alikuwa na ushawishi mkubwa kabla ya kuchaguliwa kuwa rais mwaka 2018.

Mchezo wa Kisiasa:

Nchi ya Liberia ni moja kati ya mataifa masikini duniani na bado inaendelea kutibu vidonda vya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 1989 hadi 2003 na pia janga la Ebola la mwaka 2014 hadi 2016.

Rais Weah ameshashuhudia maandamano ya kupinga hali mbaya ya uchumi chini ya utawala wake, ikiwemo pia mfumuko wa bei na uhaba wa mafuta.

Wanasiasa wa chama chake wanasema, uvumi kuhusu nia ya rais kuwania kwa muhula watatu ni mchezo wa kisiasa wakisema kiongozi wao hana nia ya kuongeza muda zaidi.

Uraia Pacha:

Hili ni suala ambalo linatarajiwa kuwa na hisia kali, kutokana na zuio la mwaka 1973 ambapo serikali ilikataza suala la uraia pacha, ingawa wengine wanaona kuwa ikiwa itaruhusiwa itafungua fursa za kiuchumi.

Katazo la uraia pacha linaonekana na baadhi ya watu kama la kibinafsi, kutokana na ukweli kuwa raia wengi wa taifa hilo wana ndugu au wazazi ambao ni Wamarekani na wanatuhumiwa kusafirusha fedha nje ya nchi kinyule cha sheria.

Mamia ya raia wa taifa hilo pia wanaelezwa kuzamia kwenye mataifa ya kigeni baada ya kukimbia vita.

Mwezi Novemba, ofisi ya rais Weah, ilisema inaamini kuzuia watu wasio raia w anchi hiyo kumiliki mali ni suala ambalo si la haki, akionesha kuunga mkono kuwa na uraia wa nchi mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.