Pata taarifa kuu
SUDAN-MAREKANI

Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan na Sudan Kusini azuru Khartoum

Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan na Sudan Kusini Donald Booth ameanza ziara yake jijini Khartoum na anatarajiwa pia kuzuru mpaka wa jimbo lenye utata la Blue Nile.

Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan na Sudan Kusini Donald Booth.
Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan na Sudan Kusini Donald Booth. eyeradio.org
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inakuja baada ya Marekani mapema mwezi huu kutangaza msaada wa Dola za Marekani Milioni 138 kwa serikali ya Juba kupitia mashirika ya misaada ya kibinadamu kuwasaidia Mamilioni ya wakimbizi ambao wameyakimbia makwao.

Akiwa jijini Khartoum, Booth anakutana na viongozi wa serikali, mashirika ya kiraia, viongozi wa kijamii na wafanyikazi wa Mashirika ya Kimataifa.

Marekani inasema ziara ya mjumbe wake itasaidia sana kujaribu kuleta waasi na serikali katika meza ya mazungumzo ili kujaribu kumaliza mzozo wa muda mrefu nchini humo.

Mapema mwezi huu mkataba wa amani uliokuwa umefikiwa kati ya makundi ya waasi na serikali ya Khartoum kuanza mazungumzo ya amani ili kumaliza mzozo katika jimbo la Darfur, ulivunjika.

Maelfu ya watu wamepoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao kutoka na makabiliano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.