Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini waendelea kuingia Sudan

Zaidi ya wakimbizi laki 2 na elfu 43 raia wa Sudan Kusini, wamewasili nchini Sudan, wakiwemo maelfu ya watu waliokuwa wakiishi kwenye jimbo lenye mapigano la Darfur, idadi ambayo imetokana na vita vilivyoanza toka mwezi December mwaka 2013, imesema taarifa ya umoja wa Mataifa.

Maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wameendelea kukimbia nchi yao
Maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wameendelea kukimbia nchi yao AFP PHOTO / UNMISS/BEATRICE MATEGWA
Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Sudan Kusini ilijitenga na kuwa huru kutoka Sudan mwaka 2011 lakini miaka miwili baadae ilijikuta ikitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya maelfu ya raia.

Wakikimbia mapigano na uhaba mkubwa wa chakula kwenye nchi yao, maelfu ya raia pia wameomba hifadhi kwenye mataifa mengine jirani ikiwemo Kenya na Uganda.

Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuendelea kwa mapigano kwenye taifa hilo, na kuongeza kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi ikiwa misaada ya dharula haitapelekwa nchini humo.

Haya yanajiri wakati huu, aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais na kiongozi wa waasi Riek Machar, akiwa mjini Khartoum, Sudan akipatiwa matibabu kutokana na kutembea umbali mrefu.

maelfu ya raia wa Sudan Kusini wanaendelea kuyakimbia makazi yao kutokana na hofu iliyoko mjini Juba, huku upande wa waasi wa Riek Machar ukiapa kufunga safari kuelekea Juba kumng'oa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.