Pata taarifa kuu
MAREKANI-KENYA

Kerry zirani Kenya kujadili mzozo wa Sudan Kusini

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry ambaye ameanza ziara yake barani Afrika, amewasili nchini Kenya na leo atakutana na Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Afrika Mashariki kujadiliana kuhusu mzozo wa Sudan Kusini na baadaye kukutana na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anayefanya ziara nchini Kenya
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anayefanya ziara nchini Kenya REUTERS/Evan Vucci/Pool
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani juma lililopita ilisema lengo kuu ya ziara hii itakuwa ni kujadili ushirikiano wa maswala ya mbalimbali hasa usalama kati ya Washington DC na mataifa hayo ya Afrika.

Mbali na suala la usalama, Kerry na rais Uhuru Kenyatta watajadiliana kuhusu ushirikiano wa kibiashara na kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Mzozo wa Sudan Kusini pia utajadiliwa katika mkutano wa viongozi hao wakati huu Umoja wa Mataifa ukitarajiwa kutuma kikosi cha kulinda amani cha wanajeshi 4,000 jijini Juba.

Siku ya Jumanne, Kerry atakutana na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari jijini Abuja, kujadili mbinu za kuwashinda magaidi wa Boko Haram ambao wamesababisha vifo vya maelfu ya watu tangu mwaka 2009 na kusababisha maelfu kuyakimbia makwao.

Mbali na ugaidi, maswala ya haki za binadamu, ufisadi na uchumi yatajadiliwa pia kabla ya Kerry kuzuru mji wa Sokoto Kaskazini mwa nchi hiyo kuzungumzia umuhimu wa amani na dini.

Nchini Saudi Arabia, Kerry atajadili mzozo wa Yemen, Syria na vita dhidi ya kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.