Pata taarifa kuu

Kenya na Tanzania, zilizokumbwa na mvua kubwa, zajiandaa kukabiliana na kimbunga

Kenya na Tanzania zinajiandaa kuwasili kwa kimbunga Hidaya siku ya Alhamisi baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Afrika Mashariki na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 350 na maelfu ya wengine kuyakimbia makazi yao.

Baadhi ya mataifa ya Afrika yameanza kushuhudia mvua kubwa inayosababisha mafuriko
Baadhi ya mataifa ya Afrika yameanza kushuhudia mvua kubwa inayosababisha mafuriko © Monicah Mwangi / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mafuriko ambayo tayari yamegharimu maisha ya zaidi ya watu 188 nchini Kenya tangu mwezi Machi pia yamesababisha watu 165,000 kuyahama makazi yao na 90 hawajulikani walipo, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema. Serikali imewataka wananchi kuendelea kuwa waangalifu.

"Ukanda wa pwani huenda ukakumbwa na Kimbunga Hidaya, ambacho kitaleta mvua kubwa, mawimbi makubwa na upepo mkali ambao unaweza kuathiri shughuli za baharini katika Bahari ya Hindi," ofisi ya Rais wa Kenya William Ruto imetangaza.

Nchi jirani ya Tanzania, ambako takriban watu 155 wamefariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi, pia inatarajiwa kuhisi nguvu ya kimbunga hicho. "Kimbunga Hidaya (...) kinatarajiwa kuathiri hali ya hewa nchini, hasa kutokana na mvua kubwa na upepo mkali katika baadhi ya maeneo karibu na Bahari ya Hindi," Shirika la Msalaba Mwekundu la Tanzania limesema kwenye X.

Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ni miongoni mwa maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na mvua kubwa katika muda wa siku mbili zijazo, mamlaka ya hali ya hewa imetangaza kwenye mtandao huo wa kijamii.

Tangu kuanza kwa msimu wa mvua nchini Kenya, mvua kubwa iliyosababishwa na mfumo wa hali ya hewa uiitwao  El Niño, imesababisha mafuriko makubwa, na kusababisha uharibifu wa barabara, madaraja na miundombinu mingine.

Wakati wa tukio baya zaidi, makumi ya watu walikufa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wakati bwawa la asili katikati mwa nchi lilipopasuka kwa sababu ya mvua kubwa.

Ushauri wa kusafiri

Marekani na Uingereza zimetoa tahadhari za kusafiri nchini Kenya, na kuwataka raia wao kuchukua tahadhari. Nchi nyingine kadhaa za Afrika Mashariki zinakabiliwa na matokeo mabaya ya mvua za msimu zilizoongezeka mara kumi na El Niño.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres "amehuzunishwa sana" kupata habari kuhusu watu kupoteza maisha katika mafuriko nchini Burundi, Kenya, Somalia, Tanzania na maeneo mengine ya Afrika Mashariki, amesema msemaji wake Stéphane Dujarric.

Nchini Burundi, takriban watu 29 wamefariki dunia na 175 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa msimu wa mvua mwezi Septemba, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema. Zaidi ya watu 237,000 waliathiriwa na mafuriko hayo, ambayo yamewakosesha makazi watu 42,000, zaidi ya nusu yao wakiwa wanawake, kulingana na chanzo hicho.

El Niño ni mfumo wa hali ya hewa ya asili inayohusishwa kwa ujumla na ongezeko la joto duniani, ambalo husababisha ukame katika baadhi ya maeneo ya dunia na mvua kubwa mahali pengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.