Kenya yakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame unaokumba Afrika Mashariki
Nchini Kenya, watu Milioni nne na laki tatu, wanakabiliwa na baada la njaa, kutokana na ukame unaoendelea kushuhudiwa, hasa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, na Shirika la msalaba mwekundu nchini humo.
Imechapishwa:
Ripoti hii inakuja, baada ya serikali ya Kenya kuruhusu uzalishaji wa vyakula vinavytokana na mazao yaliyobadilishwa vinasaba maarufu kama GMO ili kusaidia kukabiliana na hali hiyo.
Katika hatua nyingine, hatua ya serikali ya kuruhusu mazao ya GMO imepingwa vikali na wanaharakati likiwemo Shirika la Greenpeace Africa, kwa kuhofia usalama wa chakula hicho kiafya.
Serikali jirani ya Tanzania nayo imesema haitaruhusu mazao hayo kuingia katika nchi yake kutoka nchini Kenya.