Pata taarifa kuu
UKAME-TABIA NCHI

Rais Ruto aidhinisha kilimo cha mahindi yaliyobadilishwa vinasaba nchini Kenya

Rais wa Kenya William Ruto Jumatatu ameidhinisha uagizaji na ukuzaji wa mahindi yaliyobadilishwa vinasaba, ambayo yamepigwa marufuku tangu 2012, ili kukabiliana na ukame mkubwa nchini humo, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ofisi ya rais.

Rais mteule wa Kenya William Ruto, Agosti 17, 2022 jijini Nairobi.
Rais mteule wa Kenya William Ruto, Agosti 17, 2022 jijini Nairobi. REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka, zinazotaka "kufafanua upya kilimo nchini Kenya", zimetangaza kuidhinisha "mazao yanayostahimili wadudu na magonjwa".

Ofisi ya rais "imebatilisha uamuzi wake wa awali wa Novemba 8, 2012 uliopiga marufuku upanzi" wa viumbe vilivyobadilishwa vinasaba, kulingana na taarifa hiyo. “Ukulima na uagizaji wa mahindi meupe yaliyobadilishwa vinasaba sasa umeruhusiwa,” imeongeza taarifa hiyo.

Mamlaka pia inataka "kupunguza utegemezi wa Kenya" kwenye kilimo cha kutumia maji "kwa kupanda mimea inayostahimili ukame".

Akiongoza mojawapo ya matajiri wakubwa nchini, William Ruto, aliyechaguliwa mwezi Agosti mwaka huu, ameahidi kukabiliana na mfumuko wa bei unaoathiri hasa mafuta, bidhaa za chakula, mbegu na mbolea.

Mkuu huyo wa nchi, wiki moja baada ya kuingia madarakani mwezi Septemba, alikuwa amepunguza bei ya mbolea kwa nusu. Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Bw Ruto ameahidi kufufua sekta hiyo, nguzo ya uchumi ambayo ina uzito wa 20% ya Pato la Taifa.

Kenya, chombo cha uchumi wa Afrika Mashariki, inakabiliwa na ukame wa hali ya juu tangu miaka 40 iliyopita, na njaa inaathiri angalau watu milioni 4 kati ya wakazi zaidi ya milioni 50. Kulingana na mamlaka, ukame huo unaathiri kaunti 23 kati ya 47 za nchi.

Misimu minne ya mvua iliyofuatana ilisababisha hali ya ukame zaidi tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980. Mito na visima vimekauka, malisho yakawa vumbi, na kuua zaidi ya ng'ombe milioni 1.5 nchini Kenya pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.