Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Rais wa Kenya William Ruto awateua mawaziri 22 wakiwemo wanawake saba

Simon Chelugi ndiye waziri pekee aliyehudumu chini ya utawala wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta aliyeongezewa muda wa kuhudumu katika serikali hii na rais mteule.

Rais wa Kenya William Ruto wakati wa hafla ya kuapishwa Septemba 13, 2022 jijini Nairobi.
Rais wa Kenya William Ruto wakati wa hafla ya kuapishwa Septemba 13, 2022 jijini Nairobi. AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Rais mteule wa Kenya William Ruto, aliyechaguliwa mwezi uliopita, ametangaza Jumanne muundo wa serikali yake, hasa akimteua gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Kenya katika Wizara ya Fedha.

“Ninajivunia kutangaza wanaume na wanawake ambao watahudumu katika serikali,” amesema mkuu huyo wa nchi.

Ikiwa William Ruto aliahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi kuweka usawa wa kijinsia katika serikali yake, ni wanawake saba pekee waliteuliwa, kati ya jumla ya mawaziri 22.

Bw Ruto, 55, ambaye alijidhihirisha wakati wa kampeni kama mgombea wa "watu wanaofanya jitihada ya kufanikisha" na kutangaza kuwa anataka kufufua uchumi, alimteua Njuguna Ndung'u, aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Kenya, kwenye wadhifa wa Waziri wa Fedha.

Ingawa Kenya ndiyo nchi yenye uchumi unaoendelea zaidi Afrika Mashariki, inakabiliwa na matatizo makubwa, kuanzia na mlipuko wa bei za mafuta na mahitaji ya kimsingi.

Mfumuko wa bei ulifikia 8.5% mwezi Agosti, kiwango cha juu cha miaka mitano, pamoja na kushuka kwa shilingi ya Kenya, sarafu ya taifa. Tangu mwaka 2013, deni la nchi limeongezeka mara sita.

Abraham Kithure Kindiki, ambaye alimtetea Bw Ruto mbele ya Mahakama ya Juu nchini baada ya rufaa iliyowasilishwa na mshindani wake Raila Odinga, ameteuliwa katika Wizara ya Mambo ya Ndani. Aden Barre Duale ameteuliwa kwenye Wizara ya Ulinzi.

Simon Chelugi ndiye waziri pekee aliyehudumu chini ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta aliyeongezewa muda wa kuhudumu na mkuu mpya wa nchi, akihama kutoka Wizara ya Kazi kwenda ile ya Biashara Ndogo na za Kati.

Wakati wa hafla yake ya kuapishwa mnamo Septemba 13, William Ruto aliahidi "kufanya kazi na Wakenya wote".

Mahakama ya Juu ilithibitisha mnamo Septemba 5, karibu mwezi mmoja baada ya uchaguzi wa Agosti 9, ushindi wa Bw. Ruto, ambaye ni matajiri wakubwa nchini, aliongioza kwa takriban kura 233,000 (kati ya kura milioni 14) dhidi ya Raila Odinga, mtu wa kihistoria katika siasa za Kenya ambaye amekuwa akilaani ulaghai na udanganyifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.