Pata taarifa kuu

Bei ya mafuta Kenya yapanda kwa shilling 20, raia walalamika

Baada ya serikali mpya nchini Kenya kuondoa ruzuku kwa bidhaa za mafuta wiki hii, bei ya mafuta sasa imepanda kwa shilling 20 pesa za Kenya, swala ambalo limeonekana kuwa mzigo kwa raia wanaokumbwa na changamoto za kiuchumi.

Wakenya wakiwa kwenye foleni katika kituo cha mafuta cha Nairobi mwaka wa 2018.
Wakenya wakiwa kwenye foleni katika kituo cha mafuta cha Nairobi mwaka wa 2018. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Nairobi, Shughuli za uchukuzi zinaokena kuendelea kama kawaida japokuwa idadi ndogo ya magari ya kibnafsi na ya umaa yanaoenkana barabarani.

Lita moja ya mafuta ya petroli imeongezeka kwa shillingi 20 na sasa inauzwa kwa shillingi 179.30.Β 

β€œHiyo bei ya mafuta ni sisi ndio inatuumiza kama wahudumu, mwenyewe lazima apate pesa yake, askari lazima akule pesa yake kwa hivyo nyinyi mshahara wenu ndio unapunguzwa ”, amesema mmoja wa wahudumu wa magari ya umaa katika moja wapo ya vituo vya magari jijini Nairobi akihojiwa na idhaa ya Kiswahili ya RFI.

β€œ Mimi kama makanga wa matatu wakati huu tunapitia changamoto kubwa sana kwa sababu kama ile pesa mngebakia nayo kwa mfuko mafuta imechukua yote yaani maisha yamekuwa .”

Iwapo serikali ya Xilliam Ruto itanedelea na msimamo wake wa kundoa ruzuku kwa mafuta, wengi wanajiuliza ni njia ipi mbadala ya kupunguza bei ya mafuta?

Moja wapo ya ahadi za serikali ya kenya kwanza kwa wapiga kura wakati wa kampeni ilikuwa ni kupunguza bei ya mafuta, unga na kuweka mazingira bora ya kufanya Β kazi kwa wakenya swala ambalo linasubiriwa hasa wakati huu nchi hiyo ikikabiliwa na deni kubwa kitaifa kwa wakopeshaji wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.