Pata taarifa kuu

Ujumbe wa Twitter wa William Ruto: Kenya yaonyesha msimamo wake kuhusu Sahara Magharibi

Wiki iliyiopia, baada ya kuapishwa, Rais William Ruto alizua sintofahamu kwa kuchapisha na kisha kufuta ujumbe wa Twitter ambapo alionekana kutenguwa utambuzi wa Kenya kwa SADR (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi). Kutokana na hali hiyo, Nairobi imetuma barua kwa balozi mbalimbali ili kuonyesha msimamo wake.

Rais wa Kenya William Ruto wakati wa hafla ya kuapishwa Septemba 13, 2022 jijini Nairobi.
Rais wa Kenya William Ruto wakati wa hafla ya kuapishwa Septemba 13, 2022 jijini Nairobi. AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Barua hiyo ni ya Septemba 16, na inatoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya. Ujumbe wa ufafanuzi ambao unaonekana kuwa na nia ya kuwahakikishia washirika wa Kenya, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Imeandikwa katika barua hiyo kwamba Kenya "inaambatana kabisa" na azimio la Umojawa Afrika, AU, ambalo mwaka 1982 liliidhinisha kukubaliwa kwa Jamhuri ya Sahrawi ndani ya umoja huo. Kenya pia inadai kuwa inaambatana na Mkataba wa Umoja wa Afrika unaotoa "haki isiyoweza kuondolewa ya watu kujitawala".

Katika dokezo hili, Nairobi pia inakumbuha kwamba inashikamana na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la mwaka 1991 ambalo linataka "kujitawala" kwa Sahara Magharibi "kupitia kura ya maoni".

Hakuna maelezo kuhusu ujumbe wa Twitter 

Hakuna swali zaidi la kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na SADR (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sahrawi). Nairobi inathibitisha, hata hivyo, kwamba inataka kuimarisha uhusiano wake wa kibiashara na Morocco. Msimamo ambao unaweza kuonekana kuwa wa kutatanisha hadi wakati wa kiangazi, Mfalme Mohamed VI aliwaomba washirika wake kuunga mkono msimamo wake kuhusu faili hili "bila utata".

Katika dokezo hili, wizara ya Kenya hatimaye inathibitisha kwamba Nairobi "haitendi sera yake ya kigeni kwenye Twitter" bali "kupitia hati rasmi". Uchaguzi wa William Ruto kuwasilisha tangazo la umuhimu huu kwenye mtandao wa kijamii uliwashangaza wengi na kuwafanya wengine kupandwa na hasira. Bado hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa rasmi juu ya asili ya ujumbe huu wa Twitter na kufutwa kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.