Afrika Ya Mashariki
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Maadili ya viongozi wa umma nchini Tanzania
Leo tunaangazia juu ya Maadili ya Viongozi wa Umma nchini Tanzania. Tutakuwa na baadhi ya wachambuzi ambao ni Ndugu Mjungu akiwa Karagwe mkoani Kagera, pamoja na Dokta. Peter Bujari mchambuzi wa kisiasa, kiuchumi na mshauri wa sera akiwa jijini Dar es Salaam.10/08/202109:31 -
Burundi kupitia upya mikataba ya madini
Tunaangazia juu ya hatua ya Serikali ya Burundi kupitia upya mikataba ya madini lengo ikiwa ni madini ya nchi hiyo kunufaisha pande zote yaani Burundi na muwekezaji. KWa mjibu wa serikali ya Burundi, kwa sasa taifa hilo linanufaika na pato la madini aslimia 10% -15% na Burundi ingependa kiwango zaidi.03/08/202109:56 -
Utamaduni wa kuandika na kusoma vitabu nchini Tanzania
Leo tunaangazia juu ya utamaduni wa kuandika na kusoma vitabu nchini Tanzania. RFI imefika jijini Dar es Salaam kukutana na waandishi wa vitabu Bw. Yerick Nyerere pamoja na Dr. Cyrilo Christopher ambao wamejitahidi saana kuandika vitabu na kuhamasisha usomaji vitabu nchini Tanzania.27/07/202109:53 -
Changamoto za ajira kwa vijana wa nchi za Afrika Mashariki
Leo tunaangazia juu ya changamoto ya ajira kwa Vijana wa nchi za Afrika ya Mashariki, na leo tunaungana na baadhi ya vijana wa Kenya na Tanzania. Baadhi ya vijana hao wanabainisha kuwa juhudi na bidii ndio njia muafaka ya vijana kufikia ndoto zao. Vijana wanashauri vijana wenzao kutumia elimu na vipaji ili kujiinua kiuchumi.24/07/202109:43 -
Watalaam Afrika Mashariki watafuta fursa nje ya nchi zao
Leo tunaangazia juu ya changamoto ya Vijana na wataalamu wa nchi za Afrika ya Mashariki wanaofikiria kupata fursa zaidi za ajira na kipato nje ya nchi zao na bara la Afrika.15/07/202109:27 -
Historia ya mkoa wa Kigoma nchini Tanzania
Tunaangazia juu ya Mkoa wa Kigoma, nchini Tanzania. Mkoa wa Kigoma uko magharibi mwa Tanzania, kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika, ambapo Tanzania inapakana nan chi za Burundi, Jamhuri yakidemokrasia ya Congo, na Zambia.06/07/202109:53 -
Ukuzaji wa vipaji miongoni mwa vijana nchini Tanzania
Tunaangazia juu ya vipaji kwa vijana nchini Tanzania. RFI imefika tarafani Rulenge, Wilayani Ngara, mkoani Kagera magharibi mwa Tanzania na kuongea na baadhi tu ya vijana walioamua kuunda kukindi cha ‘JM Group’ kuendeleza vipaji vyao, na shughuli zao za vipaji kuwa ajiri, kuwaimarisha kiafya na kudumisha mila na tamaduni.30/06/202109:55 -
Changamoto za wanafunzi nchini Tanzania
Sekta ya elimu nchini Tanzania, inashuhudia changamoto hasa wilayani Ngara, mkoaniKagera magharibi, ikibainika kwamba walimu wanawalazimisha wanafunzi wachote maji na kuchanja kuniwakati wa muda wa masomo.Juliani Rubavu anazamia hili kwenye makala haya.24/06/202109:50 -
Utunzaji wa mazingira nchini Tanzania
Leo tunaangazia changamoto za utunzaji mazingira nchini Tanzania, tukijikita huko mkoani Kigoma magharibi mwa nchi hiyo. Kama baadhi ya wadau wa mazingira walioko wilayani Kibondo watakavyobainisha, kwasasa mazingira yanaharibiwa kwa kiwango kikubwa na kupelekea wadau kuweka wazi kilio chao.08/06/202109:55 -
Mchakato wa kuunda mkoa mpya wa Chato nchini Tanzania
Leo tunaangazia juu ya mapendekezo ya kamati ya ushauri ya mkoa wa Geita, kuunda mkoa mpya wa Chato, nchini Tanzania. Geita imependekeza mkoa mpya wa Chato uundwe na baadhi ya wilaya za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma na Shinyanga.03/06/202109:55 -
Mahusiano kati ya Watanzania na wakimbizi kutoka Burundi na DRC
Leo tunaangazia juu ya mahusiano baina ya Jamii ya Watanzania na wakimbizi wa kutokea nchi za Kongo na Burundi walioko kwenye kambi ya Nyarugusu iliyoko kwenye tarafa ya Makele, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.19/05/202109:57 -
Kupanda kwa bei ya mafuta ya kula nchini Tanzania
Leo tunaangazia juu ya uhaba na bei ghali kwa mafuta ya kula nchini Tanzania. Kwa mjibu wa serikali ya Tanzania kupitia wizara ya viwanda na biashara, viwanda vya Tanzania vinazalisha kiwango kidogo cha mafuta ya kula, hali inayopelekea wafanyabiashara kuagiza mafuta nje ya nchi.14/05/202109:55 -
Mpango wa serikali ya Tanzania kuwasaidia masikini
Tunaangazia juu ya mfuko wa kusaidia watu wasiojiweza kiuchumi nchini ujulukanao kama TASAF nchini Tanzania. Kumekuwepo na manung’uniko ya hapa na pale kuhusu wanufaikaji ambapo baadhi ya malalamiko yanataja baadhi ya watu au hata viongozi wanaojiorodheshakama wasiojiweza ili wafaidi mfuko huo.07/05/202109:49 -
Uzalishaji wa chai nchini Tanzania
Wakulima wa zao la chai katika mkowa wa Kagera, nchini Tanzania, wameshindwa kuzalisha zao hilo kutoka na changamoto nyingi, ikiwemo kukosa kupata pembejeo za zao hilo. Wengi wakiachana na ukulima wa zao hilo.Juliani Rubavu ametuandalia makala kuhusiana na changamoto za wakulima hao.27/04/202109:38 -
Hatima ya wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania
Leo tunaangazia juu ya nia ya serikali ya Tanzania kuhamasisha wakimbizi wa Burundi kurejea kwao kwa hiari baada ya kuingia nchini humo mwaka 2015 kufuatia mzozo wa kisiasa.21/04/202109:56
Afrika Ya Mashariki
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.