Afrika Ya Mashariki
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Sekta ya elimu nchini Tanzania
Makala haya ya “Afrika Mashariki”, yanaangazia sekta ya elimu kuhusu “matokeo makubwa sasa”, mpango uliyoanzishwa na serikali ya Tanzania, ambao unalenga sekta sita muhimu nchini.Ungana na Julian Rubavu...........14/01/201409:34 -
Serikali ya Tanzania yaanzisha mpango wa kuliendeleza iliyouita "matokeo makubwa sasa"
Mataifa mengi barani Afrika, yamekua yakiwataka raia kubadili tabia na kujikita na maendeleo endelevu. Serikali ya Tanzania, moja kati ya mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, imepania kutekeleza mpango wake iliyouita matokeo makubwa sasa, ambapo serikali inataka kuifanya nchi kuelekea kwenye kipato cha kati, mpango huo umelenga wizara sita, ikiwemo sekta ya elimu. Tumeongea na wadau katika mpango huo.07/01/201409:27 -
Hali ya kisiasa nchini Burundi kuelekea uchaguzi wa mwaka 20
Katika makala ya juma hili tunaendelea kuangazi ahali ya kisiasa nchini Burundi kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 hususani kuhusu changamoto za mazungumzo yanayofanyika kuelekea maandalizi ya uchaguzi huo.10/12/201309:17 -
Changamoto za kisiasa kwenye makubaliano kuelekea uchaguzi mkuu nchini Burundi
Makala hii inazungumzia changamoto za siasa kwenye mazungumzo ya kujadili makubaliano baina ya wanasiasa wa Burundi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.03/12/201309:32 -
Mfululizo wa marejeo ya makala za mwaka 2013
Msikilizaji bado tunaendelea kukuletea mfululizo wa makala zilizosikika hapa rfikiswahili kwa mwaka 2013 ambapo leo tunaangazia malalamiko ya wanawake nchini Burundi baada ya kuteketea kwa soko kuu nchini humo. Julian Rubavu anakuarifu zaidi.26/11/201309:36 -
Mtukio muhimu yaliyojiri mwaka 2013
Makala ya hii leo inaangazia matukio muhimu yaliyojiri mwaka huu ambayo kwa namna ya pekee yalipata nafasi ya kuzungumziwa katika makala zetu za mwaka huu wa 2013.19/11/201309:30 -
Sehemu ya pili ya makala ya juma lililopita ya Afrika Mashariki
Juma hili mtangazaji wa makala ya Afrika Mashariki anakuletea sehemu ya pili na ya mwisho kuhusu matumizi ya dawa za asili kwa ardhi.12/11/201309:28 -
Makala ya Afrika Mashariki
Jiunge naye Julian Rubavu katika makala haya ya Afrika Mashariki05/11/201309:26 -
Muungano mpya katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Makala ya Afrika Mashariki tunaangazia muungano wa nchi za Kenya, Uganda na Rwanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza miradi ya miundombinu bila ya kuzishirikisha Tanzania na Burundi ambazo pia ni wanachama.Ungana na Julian Rubavu kwa mengi zaidi.29/10/201309:42 -
Sehemu nyingine ya athari za biashara haramu ya gongo kiafya na kiusalama
Sehemu nyingine ya Makala ya Afrika mashariki juma hiliikiendelea kuangazia watengenezaji na walevi wa gongo na chang'aa huko Ngara Kagera Tanzania kwa namna gani Nchi yenye walevi wa gongo kupindukia inapambana na ili kupata maendeleo. Safari hii wataalamu wa Afya wanazungumzia suala hili kiafya lina madhara gani....22/10/201309:32 -
Pombe haramu na jitihada za kufikia maendeleo ya jamii Afrika mashariki
Makala ya Afrika mashariki juma hili inaangazia kuhusu watengenezaji na walevi wa gongo na chang'aa huko Ngara Kagera Tanzania kwa namna gani Nchi yenye walevi wa gongo kupindukia inapambana na ili kupata maendeleo. Ni vyema Juhudi zikachukuliwa kuzuia kabisa hilo ili rasirimali zilizopo zitumiwe kwenye mambo mengine na siyo kulewa ....karibu..!!!15/10/201309:29 -
Vijana wajiajiri Afrika Mashariki
Makala ya Afrika Mashariki wiki hii tunaangazia ukosefu wa ajira kwa vijana wa Afrika Mashariki ambao wamelazimika kujiajiri wenyewe.Julian Rubavu anaangazia suala hili.08/10/201309:30 -
Vijana wa Ukanda wa Afrika Ya Mashariki wameendelea kuwa wabunifu katika kuhakikisha wanapata ajira mpya
Vijana kutoka Nchi wanachama za Ukanda wa Afrika Ya Mashariki wameendelea kusimama kidete kubuni ajira lengo likiwa kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa ajira linalowakabili. Kamala haya yamezungumza na Vijana kutoka Tanzania na Kenya wanaoeleza namna walivyofanya juhudi katika ubunifu na kufanikisha kupatikana kwa ajira!!01/10/201309:43 -
Oparesheni kimbunga nchini Tanzania
Makala ya Afrika Mashariki juma hili inaangazia oparesheni kimbunga inayolenga kusafisha eneo la Magharibi mwa Tanzania kwa kuwarejesha makwao wahamiaji haramu na kuyafukuza makundi ya majambazi yanayotumia silaha.24/09/201309:33 -
Ujambazi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mtangazaji wa makala hii juma hili ameangazia suala la maofisa wa serikali na wajibu wa wananchi wa Jumuiya ya Afrika mashariki katika kutokomeza vitendo vya ujambazi.10/09/201309:22
Afrika Ya Mashariki
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.