Afrika Ya Mashariki
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Wahamiaji haramu bado tishio kwa nchi za Afrika Mashariki
Nchi za Afrika Mashariki na kati zinakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini moja wapo ni tatizo la wahamiaji haramu. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinaguswa na changamoto za tatizo hilo na hata kufikia kuamua kuwarudisha makwao. Leo makala ya Frika Mashariki itaangazia changamoto za kiuchumi na kijamii za kuwepo wahamiaji haramu nchini Tanzania.03/09/201309:33 -
Agizo la wahamiaji haramu kuondoka Tanzania
Makala ya Afrika Mashariki wiki hii yanaendelea kujadili agizo la serikali ya Tanzania kuwataka wahamiaji haramu kuondoka katika jimbo la Kagera na kurudi kwao.Ungana na Julian Rubavu kwa mengi zaidi.27/08/201309:32 -
Changamoto kwenye itifaki ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
Makala Yetu Ya Afrika Mashariki leo Tunaangazia juu ya changamoto kwenye itifaki ya jumuiya ya afrika ya mashariki kuhusu uhuru wa raia wa nchi tano za jumuiya hiyo kutembea na kuishi kwenye nchi za jumuiya hiyo. Je, sheria za nchi husika zikoje kuhusu suala zima la uhamiaji?Tafadhali sikiliza mwanzo hadi mwisho upate ukweli na uhakika.20/08/201309:30 -
Mahusiano baina ya maendeleo ya kiuchumi na ongezeko la maambukizi ya virus vya ukimwi (Sehemu ya nne)
Hii ni sehemu ya nne na ya mwisho ya makala kuhusu mahusiano baina ya maendeleo ya kiuchumi na ongezeko la maambukizi ya virus vya ukimwi vijijini Tanzania na nchi jirani. Maafisa wa serikali wamekuwa na mtazamo tofauti na raia kwa mazingirahatarishi yanayo sababisha ongezeko kubwa la maambukizi ya VVU. Takwimuzinazotolewa zina utata kwa ukosefu wa vifaa vya kupimia VVU.13/08/2013 -
Maendeleo na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini Tanzania
Katika makala haya leo tunaendelea na awamu ya tatu ya uhusiano kati ta maendeleo na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini Tanzania, Fuatana na Julian Rubavu.06/08/201309:21 -
Sehemu ya pili ya makala kuhusu maendeleo na maambukizi ya VVU nchini Tanzania
Karibu katika sehemu ya pili ya makala kuhusu "Maendeleo na Ongezeko la Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi VVU katika maeneo ya vijijini nchini Tanzania" sikiliza makala hii ya Afrika Ya Mashariki ukiwa naye Julian Rubavu , karibu!!30/07/201309:17 -
Maendeleo na Ongezeko la Maambukizi ya virusi vya Ukimwi vijijini Tanzania
Makala ya Afrika Ya Mashariki, juma hili tunaangazia sehemu ya kwanza ya makala kuhusu "Maendeleo na Ongezeko la Maambukizi ya virusi vya Ukimwi vijijini Tanzania". Utafiti uliofanywa na RFI ni kuwa maeneo ya vijijini kuna vituo maalumu 'center' ambapo watu hukusanyika kwa shughuli mbalimbali kuanzia asubuhi hadi usiku. Baada ya shughuli za kutwa watu hao huenda kwenye burudani ya kilevi pamoja na ngono zembe kiini cha ongezeko la maambukizi ya VVU. Hii ni sehemu ya kwanza, endelea kusikiliza juma lijalo utakaposikia wanawake na wataalamu wa afya wakizungumzia suala hili la VVU vijijini.23/07/201309:25 -
Biashara ya ukahaba kaskazini mwa Uganda
Mtangazaji wa makala haya juma hili ameendelea kuangazia biashara ya ukahaba kwenye mji wa Gulu huko kaskazini mwa Uganda.16/07/201309:30 -
Maisha ya watu wa Gulu, Uganda na mabadiliko yake baada ya vita
Uganda ni miongoni mwa nchi ambazo zimepitia mazingira ya vita kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi. Ukiangalia vita vya ndani Uganda ilikabiliana vikali na waasi wa LRA wakiongozwa na Joseph Kony. Baada ya vita hivyo, maisha ya wananchi wa Uganda yalibadilika. Katika Makala ya Afrika Mashariki leo hii tunaangazia maisha mapya ya wananchi wa huko Gulu, Uganda.02/07/201309:29 -
Wakimbizi
Hii ni sehemu ya pili ya makala kuhusu wakimbizi wa ukanda wa Afrika ya Mashariki na kati ambapo wakimbizi wa Congo na Burundi waliokimbia nchi zao wanashughulikia taratibu za kusaliriwa kama wakimbizi na kupewa haki zote za ukimbizi. Waombahifadhi na wakimbizi kwa nchini Uganda sio lazima kwao kuishi makambini kama ilivyozoeleka kwa mataifa kadhaa ya ukanda huu.25/06/201307:49 -
Vijana na ukosefu wa kazi
Makala ya Afrika ya Mashariki wiki hii yanazungumzia ukosefu wa kazi kwa vijana kutoka katika Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.Kutokana na idadi kubwa ya vijana kusoma na kutokuwa na uwezo wa kuajiriwa vijana haoa wameamua kujiajiri wenyewe na kuanzisha biashara ndogondogo kama ya usafiri maarufu kama Boda Boda.Ungana na Julian Rubavu kwa mengi zaidi.11/06/201309:23 -
Viongozi wa dini ya Kiislam nchini Uganda wajiapiza kupambana ili elimu ya dini iendelee kutolewa kwa watoto zao
Viongozi wa Dini ya Kiislam na wazazi watoto wa dini hiyo nchini Uganda wamejiapiza kuendelea kusimama kidete kupambana ili kuhakikisha watoto wanaendelea kupata elimu ya dini inayopigwa na serikali ya Kampala. Serikali ya Uganda ilitangaza kupiga marufuku uwepo wa madrasa wakisema zimekuwa zikitoa elimu ambayo ni hatari kwa ustawi wa nchi hiyo!!04/06/201309:46 -
Utalii wa Afrika mashariki na kati
Mtangazaji wa makala haya juma hili ameangazia suala utalii na changamoto zake kwenye nchi za ukanda wa Afrika mashariki.28/05/201309:21 -
Changamoto za kiusalama, kiuchumi na kijamii kwenye mpaka wa Bunagana
Leo tunaangazia awamu ya tatu ya makala kuhusu nchi ya Uganda hususani changamoto zinazopatikana kwenye mpaka wa Bunagana unaoziunganisha nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Julian Rubavu amekuandalia mengi. Karibu14/05/201309:35
Afrika Ya Mashariki
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.