Afrika Ya Mashariki
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Kupambana na ulanguzi wa binadamu Afrika Mashariki
Leo tunaangazia juu ya mapambano dhidi ya biashara, unyonywaji na usafirishaji binadamu kwenye ukanda wa afrika ya mashariki. Kwa mjibu wa mtaalamu wetu Bi. Winnie Mtevu kutoka Nairobi Kenya, vitendo hivo viovu dhidi ya binadamu vinafanywa ndani na hata nje ya mipaka ya nchi husika, ikiwa ni kinyume kabisa na haki za binadamu.11/01/202209:29 -
Matukio makubwa yaliyotokea mwaka 2021 Afrika Mashariki na Kati
Leo tunaangazia sehemu ya pili na ya mwisho ya baadhi ya makala zilizoletwa kwako mwaka uliopita wa 2021. Baadhi yake ni pamoja na utengenezaji wa nishati mbadala nchini Tanzania, uhusiano baina ya Burundi na Rwanda, wanafunzi kuagizwa kuni shule za msingi Tanzania, pia pendekezo la kuundaa mkoa mpya wa Chato nchini Tanzania.05/01/202209:52 -
Mkusanyiko wa baadhi ya matukio ya mwaka 2021
Tunaangazia sehemu tu ya baadhi ya makala zilizoletwa kwako mwaka huu wa 2021. Baadhi yake ni pamoja na uhusiano baina ya jamii ya wakimbizi na wenyeji Tanzania, Uhusiano baina ya wenyeji na raia wa Burundi na Tanzania, wasomi wa Afrika ya Mashariki kusaka ajira nje ya nchi zao, pamoja na Rushwa nchini Burundi.28/12/202109:52 -
Changamoto za mimba za watoto wa kike nchini Tanzania
Leo tunaangazia juu ya tatizo la mimba kwa watoto wa kike nchini Tanzania hususan nyakati hizi wanafunzi wawapo likizo. Baadhi ya wadau wakiwemo wazazi na viongozi wa kiroho wanaangaziatatizo hilo lilalotatiza ndoto za mtoto wa kike nchini Tanzania.22/12/202109:51 -
Changamoto za waendesha vyombo vya moto nchini Tanzania
Leo tunaangazia juu ya changamoto zinazowakumba waendesha vyombo vya moto nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee tutajikita kuongea na wadau wa magari na pikipiki huko mkoani Kagera nchini Tanzania akiangazia kuwa baadhi ya changamoto ni pamoja na ukosefu wa mafunzo ya sheria zabarabarani. Waendesha vyombo vya motona baadhi ya abiria wanaeleza uhitaji mkubwa wa elimu juu ya alama za barabarani14/12/202109:54 -
Burundi - Wafuasi wa upinzani kukamatwa
Julian Rubavu anaangazia siasa za Burundi hususan taarifa za kupotea na kukamatwa wafuasi wa vyama vya upinzani kikilengwa zaidi chama cha CNL kinachoongozwa na Agathon Rwassa.08/12/202109:58 -
Kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala nchini Tanzania
Tunaangazia juu ya uhifadhi na utunzaji mazingira nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee, RFI imetembelea kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala tofauti na uchomaji miti. Shirika lisilo la kiserikali ya REDESO (relief for development society) ndio linajishughulisha na upatikanaji wa nishati mbadala kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi wasio jiweza kambini Nyarugusu, mkoani Kigoma,30/11/202109:58 -
Uhusiano wa raia wanaoishi mpakani mwa taifa la Burundi na Tanzania
Kwenya makala haya mwandishi wetu, Juliani Rubavu, anaangazia uhusiano baina ya raia wa Tanzaniawanaoishi kwenye mpaka wa Manyovu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, najirani zao wa tarafa ya Mabanda mkoani Makamba, nchini Burundi.Wenyeji wa pande zote wanaeleza kuwa uhusiano wao ni mzuri nawanashirikiana kwa kila jambo.24/11/202109:57 -
Umuhimu wa michezo kwa wanafunzi nchini Tanzania
Leo tunaangazia umuhimu wa Michezo kwa Mwanafunzi kwa Afya ya mwili na akili. Kwenye kipindi hiki utawasikia baadhi ya wadau wakiwakilishaa makundi mbali mbali ya watoto, walezi, wazazi, na wataalamu nchini Tanzania wakiangazia umhimu wa michezo.27/10/202109:53 -
Uhuru wa kujieleza kupitia mitandao ya kijamii nchini Tanzania
Leo tunaangazia kuhusu uhuru wa kujieleza na kutoa maoni pamoja na athari za sheria ya mitandao nchini Tanzania. Kwa miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwepo na minong’ono ya hapa na pale ndani ya jamii kuhusu misingi ya kidemokrasia, uhuru wa kikatiba, na sheria za mitandao.13/10/202109:42 -
Changamoto za walemavu nchini Tanzania
Tunaangazia juu ya changamoto za ujasiriamali kwenye vikundi vya walemavu nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee tutawasikia baadhi ya walemavu na wadau wengine wanaohusika kuhakikisha mlemavu anajiwezesha kiuchumi huko mjini Bukoba, mkoani Kagera, Magharibi mwa Tanzania.05/10/202109:53 -
Fursa za vijana kujiajiri katika nchi za Afrika Mashariki
Juhudi za vijana wa ukanda wa Afrika ya Mashariki na kati ambapo licha ya changamoto za hapa na pale kiuchumi na kijamii, lakini kwa namna ya pekee baadhi ya vijana wa ukanda huu wanajibidisha kuhakikisha wanajiajiri au kuajiriwa huku wakitaja nidhamu na uaminifu kwenye jamii inayowazunguka ndio siri ya mafanikio yao.29/09/202109:50 -
Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi
Leo tunaangazia juu ya Uhusiano baina ya Burundi na Rwanda. Kwa zaidi ya miaka mitano sasa hali ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili umezorota. Baadhi ya sababu zilizotajwa na kila upande, Rwanda inataja Burundi kuhifadhi baadhi ya wahusika wa uhalifu wa kibinadamu waliokimbilia Kongo, na kwa upande mwingine Burndi inataja kwanda kuhifadhi walifanya jaribio la mapinduzi mwaka 2015.31/08/202109:49 -
Hatua ya serikali ya Burundi kuwaadhibu maafisa wake
Leo tunaangazia juu ya hatua ya serikali ya Burundi kusimamisha baadhi ya viongozi na maafisa waandamizi wa serikali iliyoko madarakani wengi wao wakiwa watumishi wa ikulu. Serikali ya Burundi ilifahamisha kwamba waliosimamishwa kazi akiwemo aliyewahi kuwa msemaji wa serikali Willy Nyamitwe na wengine, wamesimamishwa kupisha uchunguzi kwa tuhuma za kuchelewa kazini.25/08/202109:57 -
Unywaji wa pombe haramu nchini Kenya na Tanzania
Leo tunaangazia juu ya Kinywaji haramu cha ‘Gongo’ nchiniTanzania na ‘Chang’aa’ nchini Kenya. Baadhi ya wanywaji wa pande zote walioongea na RFI wanaomba serikali za nchi zao kuhalalisha kinywaji hicho cha Gondo ambapo kwa Kenya wao huiita Chang’aa, na kwa upande wa Tanzania huiita Gongo au Supu ya Mawe au Machozi ya Simba na kadhalika.17/08/202109:29
Afrika Ya Mashariki
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.