Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Burundi: Aliyekuwa Waziri Mkuu Alain-Guillaume Bunyoni kufungwa maisha jela

Nchini Burundi, baada ya siku nne za mjadala kuhusu uhalali wa kesi hiyo, upande wa mashtaka siku ya Alhamisi uliomba kifungo cha maisha jela dhidi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Alain-Guillaume Bunyoni, na kifungo cha miaka 30 jela dhidi ya washtakiwa wenzake sita. Wote wanashitakiwa kwa pamoja na mambo mengine kuhatarisha usalama wa ndani wa Serikali. Inadaiwa walipanga njama dhidi ya Rais Evariste Ndayshimiye.

Aliyekuwa Waziri Mkuu Alain-Guillaume Bunyoni kwenye mazishi ya Rais wa zamani Pierre Nkurunziza mnamo Juni 26, 2020.
Aliyekuwa Waziri Mkuu Alain-Guillaume Bunyoni kwenye mazishi ya Rais wa zamani Pierre Nkurunziza mnamo Juni 26, 2020. AFP - TCHANDROU NITANGA
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mwendesha mashtaka wa umma, Waziri Mkuu wa zamani Alain-Guillaume Bunyoni aliajiri "watu ili kumuua mkuu wa nchi" na "kupindua utawala wa kikatiba" kwa kutumia uchawi. Lakini maelezo machache yalitolewa katika kesi iliyofungwa siku ya Jumanne.

Miongoni mwa washitakiwa wenzake, anayefahamika zaidi ni DΓ©sirΓ© Uwamahoro, kamanda wa zamani wa kikosi cha kuzuia fujo. Afisa mkuu wa zamani wa huduma ya kijasusi, madereva wawili, mhandisi wa zamani wa majengo na mkuu wa kata pia wanashtakiwa.

Alain-Guillaume Bunyoni, mwenye umri wa miaka 51, ambaye mara nyingi alichukuliwa kuwa nambari 2 katika serikali iliyotokana na uasi wa zamani wa CNDD-FDD, alihifadhi nyumbani kwake pesa nyingi, kulingana na upande wa mashitaka, kwa lengo la "kuyumbisha kiwango cha ubadilishaji fedha (Faranga ya Burundi)" cha serikali.

Waziri mkuu wa zamani amekana mashtaka

Katika gereza kuu la Gitega ambapo mahakama kuu ilisikiliza kesi hiyo chini ya ulinzi mkali, mwendesha mashtaka aliomba kulipa faini maradufu kwa thamani ya "nyumba 153 na viwanja, na magari 43" vya waziri mkuu wa zamani, akihoji "mali iliyopatikana kwa njia haramu", pamoja na faranga za Burundi milioni 7.1, zaidi ya euro 2,300 kidogo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Burundi vilivyokuwepo wakati ksi hiyo ikisikilizwai, Waziri Mkuu huyo wa zamani alikana hatia, na kuhakikisha kwamba hakuna sheria "iliyomzuia kuweka pesa nyumbani kwake", na akaomba aachiliwe bila masharti, akibaini kwamba"hana hatia yoyote."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.