Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Waziri mkuu wa zamani wa Burundi afikishwa mahakamani

Waziri Mkuu wa zamani wa Burundi, Alain-Guillaume Bunyoni, amefikishwa mahakamani siku ya Alhamisi, akituhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa na kumtusi rais, chanzo cha mahakama na mashahidi wameripoti.

Waziri Mkuu wa zamani Alain-Guillaume Bunyoni kwenye mazishi ya rais wa zamani Pierre Nkurunziza mnamo Juni 26, 2020.
Waziri Mkuu wa zamani Alain-Guillaume Bunyoni kwenye mazishi ya rais wa zamani Pierre Nkurunziza mnamo Juni 26, 2020. AFP - TCHANDROU NITANGA
Matangazo ya kibiashara

Alain-Guillaume Bunyoni, ambaye alikuwa Waziri Mkuu tangu mwezi Juni 2020, alifutwa kazi mnamo mwezi Septemba 2022, siku chache baada ya rais Evariste Ndayishimiye kushutumu majaribio ya "mapinduzi ya serikali". Nafasi yake ilichukuliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Gervais Ndirakobuca.

Kwa muda mrefu Bwana Bunyoni alikuwa akichukuliwa kuwa ndiye nambari mbili wa kweli wa utawala  na kiongozi wa watu wenye msimamo mkali kati ya majenerali wanaoshikilia madaraka. Alikamatwa mwezi Aprili mwaka huu katika mji mkuu wa kiuchumi Bujumbura, siku moja kabla ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 51, na tangu wakati huo anazuiliwa katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega. Kesi ilianza mbele ya Mahakama ya Juu, ambayo ilisikizwa gerezani.

"Jenerali Bunyoni alionekana na washtakiwa wenzake sita katika chumba kilichokarabatiwa vizuri katika gereza kuu la Gitega, asubuhi ya Alhamisi kuanzia saa tano mchana hadi saa saba, mbele ya karibu watu hamsini akiwemo mmoja wa binti zake," chanzo cha  mahakama ambacho kimeombwa kutotajwa jina kimeliambia shirika la habari la AFP. Walioshuhudia wameliambia shirika la habari la AFP kwamba alikuwa amevalia sare ya kijani kibichi ambazo ni nguo wanazovaa wafungwa nchini Burundi. Kulingana na chanzo cha mahakama, alishutumu "mazingira mabaya" ya kuzuiliwa kwake.

Anashutumiwa kwa "kuhatarisha usalama wa taifa, kudhoofisha utendakazi mzuri wa uchumi wa kitaifa, na kujitajirisha kinyume cha sheria". Pia anatuhumiwa kumiliki silaha kinyume cha sheria na kumtusi rais. Mshirika wa karibu wa Rais wa zamani Pierre Nkurunziza, Bw. Bunyoni alikuwa mtu mashuhuri katika chama tawala, CNDD-FDD.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.