Pata taarifa kuu

Burundi: Waziri Mkuu wa zamani Bunyoni ashtakiwa na kufungwa kwa "kudhoofisha usalama wa serikali"

NAIROBI – Waziri Mkuu wa zamani na namba 2 madarakani, Jenerali Alain-Guillaume Bunyoni, amefungwa katika gereza la Ngozi, tangu Jumatatu Mei 8 Kaskazini mwa Burundi, baada ya kufunguliwa mashtaka rasmi Ijumaa iliopita.

Alain-Guillaume Bunyoni waziri mkuu wa zamani wa Burundi
Alain-Guillaume Bunyoni waziri mkuu wa zamani wa Burundi cds/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Alionekana amefungwa pingu, akivalia suruali na shati la kijani linalovaliwa na wafungwa nchini Burundi, Alain Guillaume Bunyoni aliingia katika mahakama ya Bujumbura akiwa amezingirwa na askari polisi waliokuwa wakimsukuma mara kwa mara kumlazimisha aende haraka. "Wale waliohudhuria kuwasili kwake hawako karibu kusahau tukio hili," alihakikishia shahidi wa RFI.

Kwa hiyo alifika mbele ya Baraza la Mahakama ya juu, ambalo lilithibitisha kufungwa kwake kwa makosa matatu ambayo muendesha mashtaka alikuwa tayari amemshtaki kwayo: "kudhoofisha usalama wa ndani wa Nchi" na "kukwamisha maendeleo ya uchumi wa taifa", vile vile. kama "kuchukua maslahi haramu". Kisha aliongezeka "umiliki haramu wa silaha na kumdharau mkuu wa nchi", bila maelezo zaidi. Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 30 jela, kulingana na wakili.

Alain-Guillaume Bunyoni, tajiri mkubwa na aliyeogopwa sana, alikuwa sehemu ya waasi wa zamani wa CNDD-FDD miaka 18 iliyopita, wa kundi ndogo la majenerali wanaotawala nchi kwa mkono wa chuma tangu kuingia madarakani kwa waasi wa zamani wa CNDD-FDD.

Akiwa amekamatwa takribani siku ishirini zilizopita katika mazingira ambayo bado hayajawekwa wazi baada ya kupekuliwa kwa kushtukiza katika nyumba zake nyingi, amehifadhiwa kwa siri hadi sasa na Idara ya Ujasusi ya Taifa (SNR), ambayo inaripoti moja kwa moja kwa rais wa Burundi.

Baada ya zaidi ya wiki mbili bila mawasiliano yoyote ya nje, aliweza kuzungumza na familia yake kwa dakika chache kabla ya kupelekwa katika gereza la Ngozi, kilomita 130 kaskazini mwa Bujumbura, ambako mrengo mzima unaokaliwa hadi sasa na wafungwa karibu mia moja walimkaribisha. Amewekwa katikza chumba cha watu wenye hadhi, chenye kitanda, choo cha kukaa, bafu na chumba cha mazoezi. Hii wakati wafungwa wengine 1,500 wanasongamana katika takriban maeneo 300 yaliyosalia, katika hali zinazoelezwa kuwa "zisizo za kibinadamu" na mashirika ya haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.