Pata taarifa kuu

Mfalme Charles III: 'Hakuwezi kuwa na kisingizio' cha dhuluma za wakoloni nchini Kenya

Hakuwezi kuwa na "kisingizio" kwa ukatili wa ukoloni wa Uingereza uliofanywa dhidi ya Wakenya, Mfalme Charles III ametangaza Jumanne hii, Oktoba 31, 2023 katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, bila hata hivyo kuomba msamaha kama walivyodai wengine.

Charles III aliweka shada la maua kwenye kaburi la askari asiyejulikana katika "Bustani ya Uhuru" ambapo bendera ya Kenya ilipandishwa mnamo Desemba 1963, badala ya "Union Jack" ya Uingereza.
Charles III aliweka shada la maua kwenye kaburi la askari asiyejulikana katika "Bustani ya Uhuru" ambapo bendera ya Kenya ilipandishwa mnamo Desemba 1963, badala ya "Union Jack" ya Uingereza. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Vitendo vya kikatili na visivyoweza kuhalalishwa vilifanywa dhidi ya Wakenya walipokuwa wakiendesha [...] mapambano makali ya uhuru na mamlaka ya Uingereza wakati wa ezi za ukoloni. Na kwa hilo, hakuwezi kuwa na kisingizio,” Mfalme huyo wa Uingereza amesema katika dhifa ya serikali iliyoandaliwa na Rais wa Kenya William Ruto.

Tume ya haki za kibinadamu nchini  Kenya (KHRC) imekadiria kuwa raia 90,000 wa Kenya waliuawa au kujeruhiwa vibaya na 160,000 kuzuiliwa wakati wa mapambano ya uhuru kati ya wapiganaji wa Mau Mau na serikali ya Uingereza wakati huo.

Wakenya wengi, walikuwa wakiangazia zaidi kile Charles walichokuwa wakichosema kuhusu dhuluma za wakati wa ukoloni, ikiwa ni pamoja na mateso, mauaji na kuenea kwa unyakuzi wa ardhi, ambayo sehemu kubwa bado inamilikiwa na  raia na makampuni ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.