Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-USALAMA

Kenya: Hali ya wasiwasi yatanda kabla ya siku kadhaa za maandamano mapya

Maandamano mengine yaliyopigwa marufuku yamepangwa kufanyika wiki hii nchini Kenya. Muungano wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga unaitisha maandamano ya siku tatu kuanzia Jumatano Julai 19 kupinga sheria mpya ya fedha na kupanda kwa gharama ya maisha. 

Kiongozi wa upinzai Raila Odinga ametangaza kufanyika kwa maandamano mapya Julai 19, 20 na 21.
Kiongozi wa upinzai Raila Odinga ametangaza kufanyika kwa maandamano mapya Julai 19, 20 na 21. AP - Samson Otieno
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu jijini Nairobi, Florence Morice

Makabiliano makali wiki jana yalisababisha vifo vya takriban watu 13 kulingana na Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya. Polisi wanatuhumiwa kurusha risasi za moto. Tangu wakati huo, wito wa mazungumzo umeendelea kutolea, bila mafanikio.

Siku ya Jumanne, Wakenya wengi wamekuwa wakijiandaa kusalia nyumbani siku nzima ya Jumatano. Na taarifa za hapa na pale kutoka mamlaka hazijabadilisha chochote. Mchana, wizara kwanza ilisisitiza kwamba Wakenya wafanye shughuli zao kama kawaida, kabla ya kutangaza jioni kufungwa kwa shule za msingi na za upili jijini Nairobi na Mombasa "kama hatua ya tahadhari".

Katika siku za hivi karibuni, taarifa za kushtumiana zimekuwa zikitolewa kwa pande zote mbili. Muungano wa Raila Odinga unashutumu serikali kwa kuwaajiri majambazi kuleta vurugu kwenye maandamano yao ambayo wanasema ni ya "amani". Mamlaka huzidisha maonyo yake na haisiti kuwashtumu waandamanaji kama "wahalifu", hata "magaidi". Shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch pia lilisema siku ya Jumanne kusikitishwa na matamshi ya baadhi ya viongozi walioonekana "kutishia" na kuwataka polisi kutumia nguvu sawia.

Mchana, wawakilishi wa kidiplomasia wa nchi 13 zikiwemo Marekani, Ujerumani na Uingereza walvunja ukimya wao na kuzitaka pande hizo mbili kufanya mazungumzo. Vyombo vya habari kadhaa vya Kenya pia vinaripoti kuhusu mazungumzo yaliyojaribiwa na kambi ya rais William Ruto, kwa lengo la kufikia mwafaka, bila mafanikio kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.