Pata taarifa kuu
MAPIGANO-USALAMA

Kenya: Raila Odinga akubali pendekezo la mazungumzo na serikali

Kiongozi wa upinzani amesitisha maandamano ya kuipinga serikali yaliyopangwa kufanyika leo Jumatatu na kukubali mazungumzo na Rais William Ruto. Kwa wiki mbili, alikuwa akiitisha maandamano mara mbili kwa wiki. Maandamano ambayo yalikumbwa na ghasia, hasa katika mji mkuu wa Nairobi.

Raila Odinga akihutubia wafuasi wake jijini Nairobi, Agosti 22, 2022.
Raila Odinga akihutubia wafuasi wake jijini Nairobi, Agosti 22, 2022. AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu jijini Nairobi, Florence Morice

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Jumapili Aprili 2, 2023 ametoa wito wa kufutwa kwa maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumatatu Aprili 3, 2023, akitangaza kwamba chama chake kitaingia kwenye mazungumzo na serikali, baada ya wiki mbili za maandamano.

"Tuko tayari kuzungumza, tunaweza kuanza kesho," alisema Raila Odinga Jumapili jioni.

Raila Odinga amesema muungano wa Azimio uko tayari kwa mazungumzo kuhusu masuala walioibua endapo serikali iko tayari kufanya majadiliano .

"Kwa kuzingatia yaliyotangulia, tunaachana na maandamano yetu ya Jumatatu, yaani kesho," Raila Odinga ameambia wanahabari. "Lakini kwa kufanya hivyo, tunataka kusisitiza kwamba haki za kukusanyika, kuandamana, kupinga na kujieleza haziwezi kuzuiwa kama inavyosema Katiba yetu".

Watu wana haki ya kufanya maandamano. Ikiwa hakuna jibu, watarejelea maandamano baada ya wiki moja. Wanasisitiza kwamba maandamano ni haki ya kimsingi iliyoainishwa katika katiba ya Kenya. Azimio tutakumbatia mazungumzo na kushirikisha timu ya Dkt Ruto kwa suluhu la amani kwa matatizo yanayokumba nchi. Azimio inataka makamishana wanne warejeshwe kazini. Azimio iko tayari kwa mchakato wa mazungumzo kuanzia kesho.

Kushughulikia gharama ya juu ya maisha. Ni sharti mojawapo lisiloweza kuondolewa kwenye orodha ya matakwa yao.

Hayo yanajiri wakati Rais wa Kenya William Ruto amemtaka kiongozi wa upinzani Raila Odinga kusitisha maandamano ya kesho na kukubaliana na mojawapo ya matakwa ya Bw Odinga ushirikiano wa pande mbili bungeni kuhusu kuundwa kwa tume mpya ya uchaguzi, IEBC.

Hata hivyo amesema hatamshirikisha Raila kuhusu matakwa yake mengine, ikiwa ni pamoja na gharama ya juu ya maisha na uhalali wa urais wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.