Pata taarifa kuu

Kenya: Odinga azionya nchi za kigeni kutoingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo

NAIROBI – Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesisitiza maandamano ya leo kufanyika kama ilivyopangwa, huku akizikosoa nchi za magharibi kwa kujaribu kuingilia masuala ya ndani ya nchi.

 Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya
Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Kauli yake anaitoa wakati huu pia Serikali ikisisitiza kutovumilia maandamano ya vurugu.

Aidha Odinga amewaonya wanadiplomasia wa kimataifa wanaojaribu kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake, akisema shida zinazoikabili nchi zitatatuliwa na wakenya wenyewe.

"Tunaambia hizo nchi zengine waachane na wakenya wasuluhishe mambo yao kama wakenya, tusifunidishwe mambo ya demokrasia na Uingereza.ameeleza Odinga."

00:13

Raila Odinga, kinara wa upinzani nchini Kenya

Katika hatua nyingine, naibu wa rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amesema uchumi wa nchi utatatizika ikiwa maandamano yanayoendelea hayatakoma, kiongozi huyu akisisitiza Serikali kutobadili msimamo.

Katika hotuba yake kwa wananchi, Gachagua amesema hawatayumbishwa na wale aliowaita wanasiasa wabinafsi wanaotaka kutumia mlango wa nyuma kuingia Serikalini.

"Machafuko yanayoelekezwa kwa raia wa Kenya na Raila Odinga yanajaribu kutusukuma kuingia katika mapatano suala ambalo haliwezekani."amesistiza Gachagua.

00:18

Rigathi Gachagua, Naibu rais wa Kenya

Haya yanajiri wakati huu rais William Ruto akiendelea na ziara yake barani Ulaya ambapo ameelekea nchini Ubelgiji baada ya kutoka Ujerumani, ambapo alisisitiza kuhusu utawala wa Sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.