Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA

Emmanuel Macron atambua jukumu la Ufaransa katika mauaji ya Rwanda

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa hotuba muhimu katika ziara yake mjini Kigali nchini Rwanda Alhamisi wiki hii ambapo amesema anatambua kwamba nchi yake ina jukumu kubwa katika mauaji ya halaiki ya mwaka nchini Rwanda.

Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Kigali mnamo Mei 27, 2021.
Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Kigali mnamo Mei 27, 2021. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kusimama kwa unyenyekevu na heshima mbele yenu, ninakuja kutambua majukumu yetu", amesema rais wa Ufaransa, wakati akithibitisha kuwa Ufaransa "haijahusika" katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Baada ya hotuba nzito kwenye eneo la ukumbusho, marais wa Ufaransa na Rwanda walijitokeza kwa mkutano na waandishi wa habari na majibu ya Paul Kagame kwa maneno hayo hayakuchelewa.

Majibu haya yalisubiriwa kwa hamu, hatimaye yamekuwa mazuri sana. "Maneno haya yana thamani zaidi kuliko kuomba msamaha, ni kweli," amesema Paul Kagame, akimaanisha hotuba ya rais wa Ufaransa kwenye ukumbusho wa Gisozi Alhamisi hii asubuhi. Rais wa Rwanda amerejelea kwa muda mrefu umuhimu wa kutambua ukweli katika uhusiano mgumu kati ya Rwanda na Ufaransa, uhusiano ambao hata hivyo umeboreshwaa atua kwa hatua katika miaka ya hivi karibuni.

Pia amemtambulisha mwenzake wa Ufaransa kama rais "anayetaka kurudisha upya na kubadilisha uhusiano wake na Afrika. "Mabadiliko yenye ubora," amesema Paul Kagame, ambaye alihitimisha: "Uhusiano kati ya nchi zetu mbili hautakuwa wa kawaida, na tumechagua kuufanikisha. "

 

Baada ya miaka hii yote ya tofauti kati ya nchi hizi mbili, itakumbukwa pia nia ya wakuu hawa wawili wa nchi za Ufaransa na Rwanda sasa kwa kufunguwa ukurasa mpya. Kufufuliwa kwa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kuligubika hotuba za viongozi hao wawili: uwekezaji wa viwanda vya Ufaransa nchini Rwanda, kurudi kwa shirika la Maendeleo ya Ufaransa nchini Rwanda na kufunguliwa tena kwa kituo cha kitamaduni cha Ufaransa.

Uteuzi wa Balozi wa Ufaransa

Emmanuel Macron pia ametangaza kwamba anakuja na dozi 100,000 za chanjo ya COVID-19 ambayo aliipa Rwanda kama sehemu ya mpango wa Covax. Bila kusahau ushirikiano wa kimahakama kati ya nchi hizo mbili kuwashtaki atu waliohusika katika mauaji ya halaiki ambao bado wako mafichoni. "Nataka kubaini kuwa kuungana huku hakubadiliki," amehitimisha Emmanuel Macron, ambaye pia ametangaza uteuzi ujao wa balozi wa Ufaransa nchini Rwanda ambaye wadhifa wake umekuwa wazi kwa miaka sita, uteuzi ambao utaidhinishwa na mamlaka ya Rwanda ameongeza rais wa Ufaransa .

Ilikuwa ni hotuba yenye nzito yenye maana maalum, amesema Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Hotuba ya Macron yakaribishwa na familia ya wahanga wa mauaji

Kiongozi wa mpito wa chama cha waathirika wa mauaji ya halaiki ya Rwanda (Ibuka), Egide Nkuranga, amesema ameridhika kabisa na hotuba ya rais wa Ufaransa: "Ni hotuba nzuri sana kwetu kwa sababu, kwanza kabisa, [rais wa Ufaransa] ametambua rasmi jukumu la Ufaransa wakati wa mauaji ya kimbari, na baada ya mauaji ya kimbari pia, ametaja wazi. Kwa hivyo hii ni nzuri sana. Amejibu ombi letu la haki, kwa sababu ameahidi kuwafikisha mahakamani wale wanaoshukiwa kuwa walihusika katika mauaji ya halaiki ambao wako huru nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.