Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA

Rwanda: Hotuba ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yasubiriwa kwa hamu

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, anazuru Rwanda kuanzia leo katika ziara ambayo inatarajiwa kuimarisha mahusiano ya mataifa hayo mawili, baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron. © Ludovic Marin/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kihistoria kwa Emmanuel Macron, ambaye anazuru Kigali Alhamisi hii, Mei 27. Emmanuel Macron ni rais wa pili tu wa Ufaransa kufanya ziara nchini Rwanda tangu mauaji ya kimbari ya Watutsi mnamo mwaka 1994.

Baada ya kudorora kwa muda mrefu uhusianokati ya Rwanda na Ufaransa, nchi hizo mbili zimeimarisha zaidi uhusiano wao katika miaka mitatu iliyopita. Wanyarwanda wengi wanasunbiri Ufaransa kuomba msamaha baada ya matukio ya mwaka 1994.

Alhamisi Mei 26, kabla ya kusafiri kwenda Rwanda, Emmanuel Macron ameelezea "imani yake kubwa" juu ya ziara yake: Rais wa Ufaransa ana hakika kuwa "ukurasa mpya utafunguliwa katika historia yetu na Rwanda na Afrika". Katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Raiswa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenyeji wake Paul Kagame watafanya mkutano na waandishi wa habari, kabla ya mazungumzo na chakula cha mchana kati ya wawili hao.

Ninaposafiri kwenda Kigali, nina imani kubwa: katika masaa machache yajayo, kwa pamoja tutaandika ukurasa mpya katika uhusiano wetu na Rwanda na Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.