Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA

Paul Kagame kukutana na wanajeshi wa zamani wa Ufaransa waliotumikia Rwanda

Rais wa Rwanda anazuru Paris Jumatatu na Jumanne. Paul Kagame anashiriki katika mikutano miwili tofauti: moja juu ya Sudan na mwingine kuhusu uchumi wa Afrika.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (picha ya kumbukumbu).
Rais wa Rwanda Paul Kagame (picha ya kumbukumbu). SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Paul Kagame anatarajiwa pia kukutana na wanajeshi wa zamani wa Ufaransa waliotumikia nchini Rwanda kati ya mwaka 1990 na 1994. Hatua nyingine katika kupanda kwa joto la uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wa Ibuka, shirika kuu la manusura wa mauaji ya kimbari, anasema wamekaribisha hatua mbali mbali zilizochukuliwa tangu kuchapishwa kwa ripoti ya Duclert na nia ya kisiasa ya serikali za Ufaransa na Rwanda, ameripoti mwandishi wetu huko Kigali, Laure Broulard.

Hata hivyo, Egide Nkuranga, kiongozi wa shirika hilo anasema anasikitisha uamuzi wa ofisi ya mashitaka ya mjini Paris wa kukataa kukubali katika uchunguzi kuhusu mwenendo wa jeshi la Ufaransa wakati wa mauaji ya Bisesero. "Tunatumahi kuwa hii itajadiliwa wakati wa ziara ya rais wa Rwanda jijini Paris," amesema.

Paul Kagame anatarajiwa kukutana na wanajeshi wa zamani wa Ufaransa waliotumikia Rwanda kati ya mwaka 1990 na 1994 na ambao kwa njia moja au nyingine walipinga sera ya Ufaransa ya wakati huo. Njia isiyo rasmi na isiyokuwa ya kawaida iliyotajwa wakati wa ziara ya Vincent Duclert mjini Kigali mwezi Aprili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.