Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA

Kagame kuhusu jukumu la Ufaransa Rwanda: "Wakati umefika wa kusamehe"

Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mahojiano maalum na RFI na France 24 amesema nchi yake na Ufaransa zina nafasi ya kuimarisha upya mahusiano yao baada ya mauaji ya kimbari yaliypotokea mwaka 1994 na kusababisha maafa ya watu zaidi ya Laki Nane wengi wakiwa Watutsi

Rais wa Rwanda Paul Kagame,katika mahojiano na RFI pamoja na France 24,Mei 17, 2021.
Rais wa Rwanda Paul Kagame,katika mahojiano na RFI pamoja na France 24,Mei 17, 2021. Β© RFI
Matangazo ya kibiashara

Rwanda katika ripoti yake, mwezi Aprili, yenye kurasa 600 ilishtumu Ufaransa kwa kutofanya lolote kuzuia mauaji hayo ya kimbari, wakati huu rais Macron akionekana kutaka kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa mara nyingine ameelezea kama "hatua kubwa ambayo imepigwa" kwa ripoti ya hivi karibuni ya wanahistoria wa Ufaransa ambayo inatambua "majukumu mazito na mabaya" ya Paris katika mauaji ya Watutsi, lakini "haikuhusika", ikifungua mlango wa kufufua uhusiano kati ya nchi hizi mbili.

"Ni hatua kubwa ambayo imepigwa (...) kwamba tunaweza kupata ukweli, ukweli, uliotolewa na tume huru. Kuna kuelewana juu ya ukweli na uthibitisho wa kile kilichotokea", Paul Kagame alisema katika mahojiano na vito vya RFI na France 24 wakati wa zaia yake jijiniParis kwa mkutano kuhusu uchumi wa Afrika ambao unafanyika leo Jumanne.

"Ufaransa na Rwanda sasa zina fursa, msingi thabiti wa kujenga uhusiano mzuri. Mambo mengine, tunaweza kuyaweka kando, labda tusisahau, lakini tusamehe", ameongeza rais wa Rwanda katika mahojiano ha ambayo yalirushwa Jumatatu jioni.

Alipoulizwa ikiwa anataka Emmanuel Macron, ambaye alizungumza naye Jumatatu na ambaye anatarajiwa wiki ijayo mjini Kigali, kuomba msamaha rasmi kwa niba ya Ufaransa, kama ilivyofanya Ubelgiji na Umoja wa Mataifa, Paul Kagame alijibu kwamba sio kazi yake ya "kumwambia mtu yeyote kuomba msamaha ".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.