Pata taarifa kuu
UFARANSA-RWANDA

Emmanuel Macron kuzuru Rwanda mwishoni mwa mwezi Mei

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza Jumanne wiki hii kuwa atazuru nchi ya "Rwanda mwishoni mwa mwezi Mei", na kuwa na "matumaini" na Rais Paul Kagame "kufunuwa ukurasa mpya katika uhusiano" kati ya Ufaransa na Rwanda.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano kuhusu  Ufadhili wa Uchumi wa Afrika huko Paris, Ufaransa Mei 18, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano kuhusu Ufadhili wa Uchumi wa Afrika huko Paris, Ufaransa Mei 18, 2021. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mahojiano maalum na RFI na France 24 alisema nchi yake na Ufaransa zina nafasi ya kuimarisha upya mahusiano yao baada ya mauaji ya kimbari yalipotokea mwaka 1994 na kusababisha maafa ya watu zaidi ya Laki Nane wengi wakiwa Watutsi

Rwanda katika ripoti yake yenye kurasa 600, mwezi Aprili, ilishtumu Ufaransa kwa kutofanya lolote kuzuia mauaji hayo ya kimbari, wakati huu rais Macron akionekana kutaka kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa mara nyingine ameelezea kama "hatua kubwa ambayo imepigwa" kwa ripoti ya hivi karibuni ya wanahistoria wa Ufaransa ambayo inatambua "majukumu mazito na mabaya" ya Paris katika mauaji ya Watutsi, lakini "haikuhusika", ikifungua mlango wa kufufua uhusiano kati ya nchi hizi mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.