Pata taarifa kuu
RWANDA

Ripoti ya Duclert: Ufaransa na Rwanda kurejesha uhusiano kamili

Baada ya ripoti ya Duclert kuwasilishwa, Ufaransa inatarajia kuimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia na Rwanda. Kwa upande wa Kigali, ambayo ilipokea ripoti hiyo kwa wakati mmoja na ikulu ya Élysée, inasema ni "hatua muhimu kuelekea ufahamu wa pamoja wa jukumu la Ufaransa katika mauaji ya watu kutoka jamii ya Watutsi".

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wa mkutano wa G7 huko Biarritz, Agosti 26, 2019.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wa mkutano wa G7 huko Biarritz, Agosti 26, 2019. © LUDOVIC MARIN / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa inabeba "majukumu mazito na makubwa" katika matukio yaliyosababisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda mnamo mwaka 1994 na ambayo yalisababisha vifo vya watu 800,000 kulingana na Umoja wa Mataifa, bila hata hivyo kuwa "kushiriki" katika mauaji hayo. Hii niitimisho kuu la ripoti ya Duclert iliyowasilishwa kwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Ijumaa.

Kwa kutambuwa jukumu la Ufaransa kwa yaliyotokea nchini Rwanda, ikulu ya Élysée ina imani kuwa "hatua mpya itapigwa katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili".

Paris inatarajia mengi kutoka kwa ripoti hii. Kwa sababu hata kama uhusiano na Kigali ulirejea kuwa mzuri tangu Emmanuel Macron aingie madarakani mnamo mwaka 2017, jukumu la Ufaransa nchini Rwanda limebaki kuwa mada hatari kwa zaidi ya miaka 25.

Mkuu wa Nchi aliagiza ripoti hii miaka miwili iliyopita kutoka kwa tume ya wataalam waliopewa jukumu la kusoma "nyaraka zote za Ufaransa zinazohusiana na Rwanda na mauaji ya Watutsi", kati ya mwaka 1990 hadi 1994, pamoja na zile zilizowekwa kama siri ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.