Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: Mapigano mapya yazuka kati ya M23 na makundi yenye silaha Kivu Kaskazini

Waasi wa M23 na makundi yenye silaha yanayoiunga mkono serikali yamekabiliana tena katika muda wa siku mbili zilizopita Mashariki mwa DRC. Kulingana na msemaji wa jeshi la Kongo katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mwanajeshi kutoka jeshi la kikanda la EAC aliuawa katika mlipuko wa bomu lililorushwa huko Kibumba. Siku ya Jumanne, mapigano hayo yalishika kasi na kusogea karibu na jiji kubwa la Goma.

Wanajeshi wa jeshi la Kongo wakiwa njiani kuelekea Kibumba Juni 2022.
Wanajeshi wa jeshi la Kongo wakiwa njiani kuelekea Kibumba Juni 2022. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu huko Goma, Coralie Pierret

Mapigano hayo yalianza alfajiri ya siku ya Jumanne, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya ndani na vya usalama, huko Kibumba, mji ulioko yapata kilomita ishirini kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini.

Mapigano haya yalitokea kati ya waasi wa M23 na makundi yanayoiunga mkono serikali. Lakini je, jeshi, ambalo linasema linaheshimu usitishaji mapigano, lilishiriki katika mapigano hayo pamoja na wanamgambo wanaoitwa wazalendo? Katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini, jeshi la FARDC linatathimini hali ya mambo na linabaini kwamba baada ya shambulio la moja ya ngome zake, "hatua zimechukuliwa kujibu matukio mashambulizi hayo".

Siku moja kabla, Jumatatu Oktoba 23, mamlaka ya Kongo ilishutumu waasi wa M23 kwa kuwaua dazeni kadhaa za raia karibu na eneo la Tongo. Madai ambayo waasi wa kundi la M23 wakanusha.

Serikali pia ilichapisha picha za ndege zisizo na rubani zinazoonyesha safu mpya ya jeshi la Rwanda lililopo DRC katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Kama ukumbusho, Kigali inashutumiwa na Kinshasa na Umoja wa Mataifa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.

Mauaji ya raia

Wakati huo huo, raia wasiopungua 26 waliuawa siku ya Jumanne katika shambulio lililohusishwa na waasi wa ADF. Usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne, washambuliaji walishambulia wilaya ya pembezoni mwa mji wa Oicha, yapata kilomita ishirini kaskazini mwa Beni.

Kulingana na mashahidi, washambuliaji hao walipora na kuua, hasa kwa visu. Kulingana na mamlaka, hawa ni wanamgambo wa ADF, kundi lenye silaha linalotoka Uganda, ambalo lilijiunga rasmi na kundi la wanajihadi la Islamic State miaka 4 iliyopita. Sasa linaendesha harakati zake katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kundi hilo lenye silaha linashutumiwa kuwaua watalii wawili wa kigeni na mwongozaji wao wiki iliyopita katika Mbuga ya Malkia Elizabeth, upande wa Uganda.

Waandamanaji wenye hasira walichoma moto magari ya mashirika a kibinadamu yaliyokuwa yakijiandaa kusambaza chakula, wakiimba: "Hatuhitaji msaada wa kibinadamu, tunataka usalama."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.