Pata taarifa kuu

DRC - Kivu Kaskazini: mji wa Kitshanga umetekwa tena na waasi wa M23

Kundi la waasi wa M23, limeripotiwa kwa mara nyingine kuudhibiti tena mji wa Kitshanga, ulioko Masisi , jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC, baada ya makabiliano makali na makundi mengine yenye silaha.

Waasi wa M23 huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Desemba 23, 2022.
Waasi wa M23 huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Desemba 23, 2022. AFP - GLODY MURHABAZI
Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya, yaliripotiwa kushika kasi tangu mwishoni mwa juma lililopita, ambapo mamia ya raia kwenye maeneo hayo walikimbia.

Kwa mujibu wa mashirika ya kiraia wilayani Masisi, waasi wa M23 walifanikiwa kuuteka mji huo hapo jana baada ya mapigano makali kati yao na wapiganaji wa makundi yenye silaha yanayounga mkono serikali.

Mwandishi wa RFI Coralie Pierret aliyeko Goma, anasema Zaidi ya wiki moja iliyopita, baadhi ya waandishi wa habari walisindikizwa hadi Kitshanga na mamlaka ya DRC kwa lengo la kushuhudia namna utulivu ulivyorejea kwenye mji huo baada ya makundi hayo kuuchukua toka kwa M23.

Jana jioni mmoja wa wasemaji wa M23 alithibitisha kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba tayari wameudhibiti mji huo, huku Jeshi la Congo likijiweka kando ya mapigano hayo kufuatia kile linasema linaheshimu usitishwaji vita dhidi ya waasi kwenye eneo hilo.

Kwa wiki kadhaa sasa, waasi hao wameendelea kupambana na wale wa Wazalendo, wanaodaiwa kuungwa mkono na wanajeshi wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.