Pata taarifa kuu

Morroco:Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la Ardhi imeongezeka na kufikia watu zaidi 2,000

Nairobi – Idadi ya watu waliofariki nchini Morroco, kufuatia tetemeko la ardhi imefikia watu, 2,122 wakati huu  shughuli za kutafuta manusura zaidi zikiendelea.

Raia wafarijiana walipokuwa wakichimba makaburi ya wahasiriwa wa tetemeko la ardhi, katika kijiji cha Ouargane, karibu na Marrakech, Morocco.
Raia wafarijiana walipokuwa wakichimba makaburi ya wahasiriwa wa tetemeko la ardhi, katika kijiji cha Ouargane, karibu na Marrakech, Morocco. AP - Mosa'ab Elshamy
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa richa 6.8, lilitokea usiku wa kuamkia jumamosi  katika maeneo yenye milima, kwa mujibu wa watalaam, huku mingine ya pwani ya Rabat, Casablanca na Essaouira yakitikiswa.Familia nyingi zikiendelea  kutafta maeneo ya kujistiri.

Familia iliyohama kwao baada ya tetemeko kubwa la Ardhi
Familia iliyohama kwao baada ya tetemeko kubwa la Ardhi AP - Mosa'ab Elshamy

Wizara ya Mambo ya ndani imesema kuwa watu wengine zaidi ya 2,421 wamejeruhiwa na wengine wengi wapo kwenye hali mbaya, na inahofiwa kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

 

Watu wanatembea kwenye mabaki yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi, katika mji wa Amizmiz, karibu na Marrakech, Morocco.
Watu wanatembea kwenye mabaki yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi, katika mji wa Amizmiz, karibu na Marrakech, Morocco. AP - Mosa'ab Elshamy

Mkurugenzi wa kitengo cha Dharura katika shirika la Madaktari wasiokuwa na Mipaka, MSF, nchini Morroco, Michel-Olivier hata hivyo ameleza changamoto wanazopita wakati huu wakiendelea na shughuli za uokozi.

Changamoto iliyokubwa kwa sasa nikuwapata majeruhi na kuwasaidia kwa pamoja.Ni eneo lenye milima na barabara nyingi hazipitiki.Inabidi kutumia farasi au pikipiki  .Amesema Michel-Olivier Mkurugenzi wa kitengo cha Dharura MSF.

00:39

MICHEL-OLIVIER MKURUGENZI MSF

Mataifa ya  Uhispania, Uingereza, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu, yameanza kutoa misaada kwa waathiriwa.

 

Mwaka 2004, watu wengine 628 walipoteza maisha na wengine 926 wakajeruhiwa baada ya tetemeko lingine kutokea katika eneo la Al Hoceima Kaskazini mwa nchi hiyo. Mwaka 1960, tetemeko lenye ukubwa wa ritcha 6.7, lilisababisha vifo vya watu 12,000 katika mji wa  Agadir.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.