Pata taarifa kuu

Mpishi wa Nigeria athibitishwa na Guinness Book of World Records

NAIROBI – Mpishi wa Nigeria ambaye amekuwa maarufu nchini humo baada ya kupika bila kukoma kwa zaidi ya saa tisini na tatu  amethibitishwa kuwa mshikilizi mpya wa rekodi ya dunia.

Mpishi wa Nigeria athibitishwa na Guinness Book of World Records
Mpishi wa Nigeria athibitishwa na Guinness Book of World Records © Guinness World Records
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa na watu mashuhuri walimshangilia Hilda Baci wakati akiwa jikoni kwake huko mjini Lagos wakati alipopika kwa  kipindi cha siku nne mwezi uliopita.

Alitumia zaidi ya sahani 100 katika mchakato huo na aliruhusiwa tu kuchukua mapumziko ya dakika tano kila saa.

Baci amemshinda mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia Lata Tondon wa India, ambaye alikuwa anashikilia rekodi hiyo kwa  muda wa saa 87 dakika 45 mwaka wa 2019.

The Guinness Book of World Records, ambao walichunguza tukio hilo la kupikika, wamempongeza kwa kupitia ujumbe wa video:

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.