Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Sudan: Marekani yatangaza vikwazo vipya 'dhidi ya wahusika wanaodumisha vurugu'

Marekani itaweka vikwazo vipya vya kiuchumi na kuwanyima visa "wahusika wanaochochea vurugu" nchini Sudan, afisa mkuu wa Ikulu ya White House ametangaza siku ya Alhamisi Juni 1, 2023. Ghasia nchini humo ni "janga" ambalo "lazima likome", Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa kitaifa wa Joe Biden amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi juu ya vikwazo hivyo.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhane (kushoto) na Jenerali Mohamed Hamdane Daglo (Kulia)
Jenerali Abdel Fattah al-Burhane (kushoto) na Jenerali Mohamed Hamdane Daglo (Kulia) © RFI
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wakimbizi 100,000 wapya wa Sudan wamekimbilia nchini Chad tangu kuanza kwa vita nchini humo, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Idadi ya Wasudan waliokimbilia nchi jirani ya Chad kufuatia mzozo wa umwagaji damu unaoendelea nchini humo kwa mwezi mmoja na nusu imezidi watu 100,000, Shirika la Umoja wa Mataifa linahudumia Wakimbizi (UNHCR) limeelezea wasiwasi wake Juni 1, 2023, likidai msaada wa dharura wa kifedha. 

"Idadi ya wakimbizi wapya imevuka kiwango cha watu 100,000" tangu mwanzoni, Aprili 15, 2023, ya mzozo kati ya majenerali wawili hasimu wanaogombea madaraka huko Khartoum, na "inakadiriwa kuwa hadi watu 200,000" zaidi wanaweza kuyatoroka makazi yao na "kukimbilia nchini Chad ndani ya miezi mitatu ijayo", anaonya Laura Lo Castro, mwakilishi wa UNHCR nchini Chad, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.