Pata taarifa kuu

Ugonjwa wa uti wa mgongo umeua zaidi ya watu 100 tangu Januari nchini Niger

Niger na Shirika la Afya Duniani (WHO) wamezindua kampeni ya chanjo dhidi ya homa ya uti wa mgongo ambayo imeua zaidi ya watu 100 tangu mwezi Januari, hasa katika eneo la Zinder (kusini), kwa mujibu wa shirika la habari la AFP likinukuu Wizara ya Afya ya Niger.

Meningococcus ni bakteria ambayo inaweza kusababisha Homa ya uli wa mgongo na aina nyingine za ugonjwa wa meningococcal.
Meningococcus ni bakteria ambayo inaweza kusababisha Homa ya uli wa mgongo na aina nyingine za ugonjwa wa meningococcal. © Shutterstock / Tatiana Shepeleva
Matangazo ya kibiashara

Homa ya uti wa mgongo tangu mwezi Januari umeua watu 102, wengi wao wakiwa watoto, kati ya viwagonjwa zaidi ya 1,810 vilivyorekodiwa, kulingana na wizara. Eneo la Zinder, linalopakana na Nigeria, ndilo lililoathiriwa zaidi na wagonjwa zaidi ya 1,470 na vifo 84, wizara hiyo imebainisha. Kulingana na televisheni ya umma, Niger na WHO wamezindua kampeni ya chanjo katika mji wa Zinder inayolenga takriban watu 380,000 kuanzia Mei 17 hadi 25.

Eneo la Zinder linapakana na jimbo la Jigawa nchini Nigeria, ambako ugojwa huo pia unaripotiwa, hivyo basi kuna "hatari ya ugonjwa huo kusambaa katika nyingi jirani", ilitahadharisha WHO mapema mwezi Februari.

"Jambo jingine, kuonekana kwa wakati mmoja kwa magonjwa mengine ya milipuko, ukosefu wa usalama na kuhamishwa kwa raia, yote katika muktadha wa mzozo wa muda mrefu wa kibinadamu, kunaweza kuchangia kuenea kwa mlipuko katika nchi zingine za ukanda mdogo wa Afrika Magharibi", WHO imesema.

WHO inatathmini hatari inayoletwa na mlipuko wa sasa wa homa ya uti wa mgongo nchini Niger kuwa ya juu katika ngazi ya kitaifa, ya wastani katika ngazi ya kanda na ya chini katika ngazi ya kimataifa.

Niger mara kwa mara hukumbwa na milipuko ya ugonjwa wa uti wa mgongo kutokana na nafasi yake ndani ya "ukanda wa uti wa mgongo barani Afrika", unaoenea katika bara zima, kutoka Senegal magharibi hadi Ethiopia mashariki. Nchini Niger, ugonjwa huo uliua karibu watu 200 mwaka 2017, hasa watoto. Mnamo 2015, homa ya uti wa mgongo iliua watu 577 kati ya wagonjwa zaidi ya 8,589.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.