Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Zaidi ya watu 100 wauawa katika mapigano ya kikabila nchini Nigeria

Zaidi ya watu 100 wameuawa wiki hii katikati mwa Nigeria kutokana na mapigano ya kikabila yanayoendelea, ambayo yamewalazimu maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao, mamlaka ya eneo hilo imesema leo Ijumaa asubuhi.

Jimbo la Plateau limeendelea kushuhudia visa malimbali vya uhalifu, mauaji na utekaji nyara.
Jimbo la Plateau limeendelea kushuhudia visa malimbali vya uhalifu, mauaji na utekaji nyara. © KOLA SULAIMON/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la kitaifa la usimamizi wa dharura, zaidi ya watu 3,000 wamelazimika kuyahama makazi yao na mamia ya nyumba kuharibiwa.

Tangu Jumatatu jioni, mashambulizi ya watu wenye silaha kwenye vijiji kadhaa katika wilaya ya Mangu (jimbo la Plateau) "yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100", mwakilishi wa wilaya ya Mangu, Daput Minister Daniel ameliambia shirika la habari la AFP.

Ripoti ya awali siku moja kabla iliripoti watu 85 waliuawa na makumi waliojeruhiwa kulazwa hospitalini.

Mikoa ya kaskazini-magharibi na kati ya Nigeria mara kwa mara ni eneo la mivutano na mizozo mibaya kutokana na utumiaji wa ardhi na rasilimali za maji kati ya jamii za wakulima na wafugaji, iliyochochewa katika miaka ya hivi karibuni na shinikizo la idadi ya watu na mabadiliko ya tabia nchi.

Mfululizo wa mauaji yanayofuatiwa na ulipizaji kisasi umesababisha uhalifu mkubwa katika mkoa huo, huku magenge ya watu wakiendesha msafara uliolengwa katika vijiji, ambapo wanaua wakazi kwa makumi, wakipora mali na kujihusisha na utekaji nyara kwa kutarajia fidia.

Siku ya Alhamisi, polisi ilisema kuwa vikosi vya usalama viliwekwa katika eneo hilo, na kwamba watu watano kuhusiana na vurugu hizo wamekamatwa, na kwamba utulivu umerejea.

Lakini mchana, vyanzo kadhaa vya ndani vililibainishia shirika la habari la  AFP kwamba ghasia ziliendelea.

"Kufikia sasa, mashambulizi na visa vya nyumba kuchomwa moto vimeripotiwa katika maeneo mengi," afisa wa eneo hilo Bw. Daniel amesema Ijumaa asubuhi.

"Tunahitaji zaidi watu kutulindia usalama, kutoka kwa jeshi na jeshi la anga, kutusaidia kuwakimbiza washambuliaji," amebaini, akiongeza kuwa watu wengine wapya wameyatoroka makaazi yao na vijiji.

"Nyumba zimechomwa moto, watu sasa wametawanyika kila mahali, wengine wako makanisani, misikitini na sehemu zingine salama."

Siku ya Alhamisi, shirika la kitaifa la kusimamia Dharura (NEMA) lilisema kwamba zaidi ya watu 3,000 wamelazimika kuyahama makazi yao na mamia ya nyumba kuharibiwa.

Serikali ya Jimbo la Plateau hadi sasa haijatoa tathmini sahihi, ikitangaza tu, katika taarifa kwa vyombo vya habari Ijumaa asubuhi, "vifo vingi" katika ghasia hizo.

Alhamisi jioni Gavana Simon Lalong aliitisha mkutano wa dharura kuhusu mashambulio hayo na kusema vikosi vya usalama vitadumisha uwepo wake ili kukomesha ghasia zaidi, ilisema taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.