Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Makumi ya waumini wa Kikatoliki wauawa na watu wenye silaha nchini Nigeria

Mauaji hayo yalifanyika baada ya misa ya Dominika ya Pentekoste, katika mji mdogo katika jimbo la Ondo, kusini-mashariki mwa Nigeria, eneo ambalo halijaokolewa hadi wakati huo na ghasia ambazo zilisababisha maeneo mengine ya nchi kukumbwna jinamizi la mauaji.

Waumini wa Kikatoliki huko Lagos.
Waumini wa Kikatoliki huko Lagos. PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Milio ya risasi ya kwanza ilisikika mchana wakati waumini walipoanza kuondoka katika Kanisa la Mtakatifu Francis huko Owo, mji mdogo ulio zaidi ya kilomita 300 mashariki mwa mji wa Lagos. Milipuko ya mabomu na milio ya risasi vilisikika, na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha, wanasema mashahidi walionukuliwa na vyombo vya habari vya Nigeria.

Manusura wa shambulio hilo wamesema walisubiri takriban dakika 20 kabla ya majeruhi kuanza kubebwa hospitalini. Daktari aliyenukuliwa na shirika la habari la Reuters alikadiria siku ya Jumapili kuwa "sio chini ya miili 50" ililetwa katika hospitali za mji huo.

Askofu na gavana wa jimbo hilo mara moja walikwenda kwenye eneo la tukio. Gavana wa jimbo hilo alitaja tukio hilo kama" shambulio "mbaya na la kishetani". Papa Francis mwenyewe, huko Roma, alifahamisha kwamba "aliombea waathiriwa wa tukio hilo". Rais Muhammadu Buhari, alilaani shambulio hilo na kusena ni uhalifu usiokubalika".

Mkoa huu ulikuwa umetengwa na ghasia katika miaka ya hivi karibuni, ingawa umekuwa ukikumbwa na ongezeko la mashambulizi kati ya wakulima na wafugaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.