Pata taarifa kuu

Senegal: Chama cha madaktari chaitisha mgomo baada ya wafanyakazi wa afya kukamatwa

Kisa cha mwanamke na mtoto wake mchanga, waliofariki wakati wa kujifungua huko Kédougou, kusini-mashariki mwa nchi, kinaendelea kuzua sintofahamu. Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili, chama huru cha Madaktari nchini Senegal kiliitisha mgomo wa saa 48 kuanzia Jumatatu hii, Septemba 5, kutaka wahudumu watatu wa afya waliokamatwa kuachiliwa.

Hospitali ya jimbo la Amath Dansokho huko Kédougou, Senegal.
Hospitali ya jimbo la Amath Dansokho huko Kédougou, Senegal. © RFI/Théa Ollivier
Matangazo ya kibiashara

Taasisi zote za afya nchini Senegal zitagoma kwa saa 48 kuanzia Jumatatu hii, Septemba 5. Katibu mkuu wa chama huru cha madaktari, Amadou Yeri Camara, alisema aliomba kuachiliwa kwa daktari wa magonjwa ya wanawake, daktari wa ganzi na muuguzi walioshtakiwa kwa mauaji kufuatia kifo cha mama na mtoto wake mchanga.

"Kama madai yetu hayatapatiwa ufumbuzi, tutaendelea na msimamo huu. Hatutakubali kuwaweka madaktari gerezani kwa ndiyo au hapana. »

Wizara ya Afya ilieleza kwa kina katika taarifa mpangilio wa matukio hayo ulioanzishwa kutokana na ukaguzi uliofanywa. Hati inayowaondolea mashtaka wahudumu watatu wa afya waliokamatwa, kulingana na Dk. Ibrahim Aidibé, rais wa Chama cha Madaktari wa Magonjwa ya Wanawake (ASGO).

Alipinga pia taarifa ya mwendesha mashitaka, ambayo inaibainisha "uzembe mkubwa wa matibabu". “Hatukatai kufunguliwa kwa uchunguzi wa kimahakama, lakini tunataka taratibu zifuatwe. Vipengele vyote vya ukweli vinaenda kinyume na shutuma ambazo zimetolewa dhidi ya timu ya utunzaji. Kwa kuwanyima uhuru maafisa hao, mwendesha mashtaka ameacha chumba cha upasuaji katika mazingira magumu, bila kusubiri ripoti kuhusiana na uchunguzi kwa vipimo vya damu na mifupa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.