Pata taarifa kuu

DRC: Madaktari wagoma kudai mazingira bora ya kazi

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Chama cha Madaktari (Synamed) kiko kwenye mgomo kwa miezi kadhaa. Wiki hii, madaktari waliamua kuimarisha harakati zao kwa kuanzisha operesheni "hospitali zisizo na madaktari". Wanadai mazingira bora ya kazi, lakini juu ya yote kuheshimisha ahadi zilizotolewa na serikali za kuongeza mishahara yao.

Hospitali Kuu ya Makala iliyoko jijini Kinshasa, DRC.
Hospitali Kuu ya Makala iliyoko jijini Kinshasa, DRC. © RFI/ Ophélie Lahccen
Matangazo ya kibiashara

Katika hospitali kuu ya mji mkuu Kinshasa, vitanda katika vyumba kadhaa vya matibabu vimejaa wagonjwa. Madaktari wachache waliopo huzunguka na kuchukua zamu kwa karibu miezi miwili kufanya huduma hiyo.

“Wagonjwa wanaolazwa hospitalini wanahudumiwa na wakuu wa idara na wakuu wa huduma. Sisi, Synamed, hatupokei wagonjwa tena,” anaeleza Dk. Aimé Umba, mmoja wa wasimamizi wa chama ha madaktari, Synamed, wa hospitali hii ya umma, kubwa zaidi jijini Kinshasa.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi, Daktari Fabien Nzoko, anaishtumu serikali kuhusika na hali hiyo: “Ni serikali kuwasogelea madaktari kwa kuzingatia dhiki ya watu, amebaini. Sio kila mtu anayeweza kumudu matibabu nje ya nchi au katika hospitali za kibinafsi. Serikali ndio inahusika na kile kinachotokea kwa raia wa DRC. "

Kiini cha mzozo huo, utekelezaji wa makubaliano yaliyotiwa saini kati ya wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi na serikali mnamo Agosti 3, 2021 kuhusu mazingira ya kazi ya madaktari. Madaktari wanadai, miongoni mwa mambo mengine, posho za usafiri na malazi, kama ilivyojadiliwa.

"Kwa madaktari wapya, serikali imejitolea kulipa faranga 400,000 za Kongo kila mwezi, sawa na dola 200, ameongeza Dk. Aimé Umba.

Kwa upande wake, serikali imetangaza kufanyika katika siku zijazo kile kinachoitwa warsha ya kuoanisha maoni ili kukamilisha mazungumzo na kuepuka kuzorota kwa sekta ya afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.